Iran yasisitiza tena kukataa mazungumzo na Marekani mpaka nchi hiyo itakapoondoa vikwazo
Rais Hassan Rouhani wa Iran amesisitiza tena kuwa, hatafanya mazungumzo na Marekani isipokuwa ncho hiyo ikiondoa vikwazo dhidi ya Iran.
Akihutubia mjadala wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa, rais Rouhani amesema serikali na watu wa Iran wana msimamo thabiti dhidi ya vikwazo vikali vilivyowekwa na Marekani katika mwaka mmoja na nusu uliopita, na kamwe Iran haitafanya mazungumzo na adui anayetaka kuifanya ijisalimishe kwa kutumia silaha ya umaskini, shinikizo, na vikwazo.
Rais Rouhani amehimizwa na viongozi mbalimbali haswa rais Emmanuel Macron wa Ufaransa kukutana na rais Trump wa Marekani kando ya mkutano wa Umoja wa Mataifa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |