Georgieva wa Bulgaria ateuliwa mkurugenzi wa IMF
Bodi ya utendaji ya Shirika la Fedha la Kimataifa IMF imeidhinisha uteuzi wa Kristalina Georgieva raia wa Bulgaria aliyekuwa ofisa mtendaji wa Benki ya Dunia, kuwa mkurugenzi wa shirika hilo kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia Oktoba Mosi.
Bibi Georgieva amesema ni heshima kubwa kwake kuteuliwa kama mkurugenzi wa IMF, hata hivyo ametambua changamoto kubwa inayomkabili, kwamba ukuaji wa uchumi wa dunia ni dhaifu, mvutano wa kibiashara unaendelea, na mzigo wa madeni unaongezeka katika nchi nyingi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |