Wahudumu wa afya katika gereza moja mjini Bukavu mashariki mwa Jamuhuri ya kidemokrasia ya congo wamesema kuwa wafungwa wapatao 45 wamefariki dunia tangu mwanzo wa mwaka huu kutokana na ukosefu wa matibabu. Wangonjwa wengine walipelekwa hosptali kuu lakini hakukua na huduma za kutosha. Hali hiyo imewafanya timu ya madaktari katika gereza hilo kugoma kufanya kazi nakuomba serekali kuimarisha hali sio tu ya afya lakini pia ya maisha mazuri kwa wafungwa maeneo hayo. Lakini kikubwa ni hali mbaya ya huduma ya sio tuu ya afya bali pia mateso mengine wanayopitia wafungwa katika magereza wakiomba serikali kuboresha hali hiyo.
Tangu mwezi Januari mwaka huu hadi sasa zaidi ya wafungwa 45 wamefariki dunia kutokana na ukosefu wa matibabu katika gereza hilo. Hata hivyo wafungwa 325 wanaugua ugojwa wa utapiamlo, 13 wakiwa na virusi vya HIV huku 23 wakiugua ugonjwa wa kifua kikuu. Wanaharakati wa haki za kibinadamu wamesema kuwa lazima serekali isikilize wauguzi hao wa gereza hilo na kuchukua hatua za haraka.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |