• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Oktoba 12-Oktoba 18)

    (GMT+08:00) 2019-10-18 19:20:18

    Tanzania: Mfanyabiashara aliyetajwa kuiibia Tanzania Tsh. Milioni 7 kila dakika, aachiliwa huru

    Mfanyabiashara maarufu nchini Mohamed Yusufali, Aliyekuwa akikabiliwa na kesi mbili za uhujumu uchumi na kukwepa kodi na kuisababishia Serikali hasara ya Tsh. bilioni 27 kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Ameachiwa huru na Mahakama baada ya maafikiano na Mkurugenzi wa mashtaka. Mfanyabiashara huyo ambaye aliwahi kutajwa na Rais Magufuli kuwa, Alikuwa akiibia Serikali ya tanzania Tsh. milioni 7 kwa dakika kupitia mashine za kodi za kielektroniki (EFD), alitoka juzi Oktoba 16, 2019 na wenzake baada ya kukaa mahabusu kwa miaka mitatu kutokana na mashtaka ya utakatishaji fedha.

    Yusufali ameachiwa baada ya kukamilisha mchakato wa msamaha wa Rais kisheria mahakamani kwa mujibu wa makubaliano yake na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) katika kesi ya pili ya utakatishaji fedha iliyokuwa inamkabili.


    1  2  3  4  5  6  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako