Bondia Patrick Day aliyepigwa na kupoteza fahamu afariki dunia
Bondia wa Marekani Patrick Day Amefariki dunia siku ya jumatano katika hospitali ya Northwestern Memorial nchini humo, baada ya kupigwa akiwa ulingoni katika roundi ya 10 na mpinzani wake Charles Conwell siku ya Jumamosi. Patrick aliyekuwa na miaka 27 alipata majeraha makubwa katika ubongo na kumsababishia kupoteza fahamu.
Charles Conwell aliyekua mpinzani wake aliandika kwenye kurasa wake wa Twitter akisema "nilikuwa nataka kushinda tu. Kama ningeweza kurudisha muda basi ningerudisha. Hakuna mtu anayestahili hili kutokea kwake." Mungu ampumzishe Patrick mahala pema peponi.Bondia Patrick Day alianza masumbwi mwaka 2013 alikuwa ameshinda mapambano 17 (6 kwa KO), kapigwa manne(4) na sare moja katika mapambano yake yote 22 aliyocheza kabla ya pambano la Jumamosi alilo pambana na Charles Conwell ambapo alipigwa makonde mazito kwa kasi kali iliyopelekea mauti yake. Baadhi ya mabondia waliofariki katika kipindi cha miezi 6 iliyopita kufatia majeraha ya kupigwa ulingoni:
Hugo Santillan (Argentina)
Boris Stanchochov (Bulgaria)
Maxim Dadashev (Russia)
Patrick Day (USA)
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |