Uzinduzi wa reli mpya ya SGR awamu ya pili.
Kenya imezindua awamu ya pili ya ujenzi wa gari moshi ya kisasa ya standard GAUGE itakaogharimu dola za kimarekani bilioni 1.5.
Reli hiyo ya abia itaanzia safari zake kutoka Nairobi kwenda eneo la Bonde la Ufa huko mjini Naivasha .
Kwa mujibu wa mamlaka za Reli nchini humo, ujenzi wa awamu nyingine ya reli hiyo kwa ajili ya mizigo utafanyika hapo baadae kufuatia kuchelewa kwa marekebisho ya reli ya zamani kuelekea Uganda na bandari ya nchi kavu katika eneo la Naivasha. Ujenzi wa awamau ujenzi wa reli mpya ya kisasa umekuwa ukiendeshwa na kampuni ya Kichina ya Chinese Communications Construction Company. Awamu hii ya pili ya SGR itaunganisha kaunti tano, zikiwemo Nairobi, Kajiado, Narok, Kiambu na Nakuru. Vile vile, kutakuwa na vituo vinne vya abiria ambavyo ni Ongata Rongai, Ngong, Mai Mahiu na Suswa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |