Virusi vya corona huenda "visiishe"limeonya Shirika la Afya Duniani(WHO), Akizungumza katika kikao Jumatano, Mkurugenzi wa dharura wa WHO, Dkt Mike Ryan ameonya dhidi ya kujaribu kubashiri ni lini virusi vya corona vitatoweka.
Aliongeza kuwa kama chanjo itapatikana, kudhibiti virusi kutahitaji"juhudi kubwa",
Takribani watu 300,000 kote duniani wameripotiwa kufa kutokana na virusi vya corona, na zaidi ya visa milioni 4.3 vimerekodiwa.
Kwa sasa kuna chanjo zaidi ya 100 zainazofanyiwa utafiti- lakini Dkt Ryan amesema kuna magonjwa mengine, kama vile tetekuwanga, ambayo bado hayajatokomezwa licha ya kuwa kuna chanjo yake.
Mkurugenzi Mku wa Tedros Adhanom Ghebreyesus alisisistiza kuwa bado inawezekana kudhibiti virusi vya corona, kwa juhudi.
Kauli zao zinakuja huku nchi mbalimbali zikianza kulegeza hatua za kukaa nyumbani, na viongozi wanaangalia uwezekano wa lini na ni vipi wanaweza kufungua shughuli za kiuchumi katika nchi zao.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |