Virusi vya Corona: Kituo cha kudhibiti magonjwa cha AU chaitaka Tanzania kutoa takwimu
Kituo cha kudhibiti magonjwa barani Afrika (Africa CDC) kilichopo chini ya Umoja wa Afrika (AU) kimeitaka Tanzania kutoa takwimu mpya za mwenendo wa ugonjwa wa corona nchini humo.
Mkurugenzi wa Africa CDC, Dkt John Nkengasong, siku ya Alhamisi wiki hii, amesema kuwa kituo chake kwa kutumia takwimu hizo kipo tayari kushirikiana na Tanzania kwa kuipatia msaada wa kitaalamu na kiufundi unaohitajika.
Kwa ujumla wake, Africa CDC imesema inazitaka nchi zote kutoa takwimu kwa haraka kwa kuwa hicho ndicho kiungo muhimu katika kuendesha vita dhidi ya mlipuko wa corona.
Dkt Ngasong ametahadharisha kuwa, kwa baadhi ya nchi kuamua kutotoa takwimu kunatengeneza wasiwasi kwa nchi nyengine.
Mara ya mwisho kwa Tanzania Bara kutangaza takwimu mpya za corona ilikuwa wiki mbili zilizopita Aprili 29, huku Zanizbar ikitoa takwimu mpya kwa mara ya mwisho wiki moja iliyopita Mei 7.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |