• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Mei 9-Mei 15)

    (GMT+08:00) 2020-05-15 20:33:10

    Uchaguzi wa Burundi 2020: Kwanini Burundi imewatimua maafisa wa WHO?

    Shirika la Afya duniani (WHO) liko katika harakati za kuwahamisha wafanyikazi wake wanne kutoka nchini Burundi baada ya kuambiwa waondoke na serikali.

    Mkurugenzi wa kieneo barani Afrika Daktari Matshidiso Moeti, amethibitisha habari hiyo kwenye mkutano na waandishi wa habari, lakini akaongeza kuwa hajui ni kwanini viongozi walichukua hatua hiyo.

    Hata hivyo Dk Moeti amesema kuwa licha ya kufukuzwa bado WHO itashirikiana na viongozi wa Burundi katika kukabiliana kwao na janga la virusi vya COVID19.

    Hatua hiyo inajiri baada ya ujumbe kutoka kwa wizara ya mambo ya nje nchini Burundi, uliotumwa mtandaoni kuwataka wawakilishi wa Shirika la Afya Duniani kuondoka nchini humo ndani ya saa 48.

    Dkt. Walter Kazadi Mulombo ambaye alikuwa mwakilishi wa WHO nchini Burundi pamoja na wataalamu wengine Pr. Tarzy Daniel, Dkt. Ruhana Mirindi Bisimwa na Dkt. Jean Pierre Murunda Nkatawana wamepatiwa hadi Mei tarehe 15 kuondoka.

    Katika mahojiano ya simu, na shirika la habari la BBC, Waziri wa mambo ya nje wa Burundi Ezechiel Nibigira hakukataa wala kuthibitisha hatua hiyo.

    Serikali ya Burundi inakabiliwa na ukosoaji mkubwa kwa kuandaa uchaguzi katika mazingira ya janga la corona, licha ya kuripoti kuwa na wagonjwa 27 na kifo cha mtu mmoja.

    Kampeini ya wagombea urais zinafanyika kote nchini humo kabla ya uchaguzi utakaofanyika Jumatano, bila ya kuwa na utaratibu wa kukabiliana na maambukizi ya virus ya corona.

    Hali hiyo imezua hofu ya kusambaa kwa virusi via ugonjwa wa Covd-19 katika taifa hilo dogo la Afrika Mashariki.


    1  2  3  4  5  6  7  8  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako