Zaidi ya wabunge 300 duniani waitaka IMF, Benki ya Dunia kufuta madeni ya nchi masikini
Zaidi ya wabunge 300 kutoka duniani kote wamelitaka leo shirika la fedha ulimwenguni IMF na benki ya dunia kufuta madeni ya mataifa masikini kutokana na janga la virusi vya corona, na kuongeza hatua ya kuzipatia fedha ili kuepuka mdororo wa kiuchumi duniani.
Juhudi hizo, zikiongozwa na mgombea wa zamani wa kiti cha urais nchini Marekani seneta Bernie Sanders na mbunge wa baraza la wawakilishi Ilham Omar, wa chama cha Democratic kutoka jimbo la Minnesota, zinakuja wakati kuna wasi wasi mkubwa kwamba mataifa yanayoendelea pamoja na masoko yanayoinukia yataathirika kwa kiasi kikubwa kutokana na janga la virusi vya corona.
Virusi hivyo vimeaambukiza watu zaidi ya milioni 4.2 duniani na huku watu takriban laki tatu wakipoteza maisha yao. Haya ni kwa mujibu wa idadi iliyokusanywa na shirika la habari la Reuters.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |