Msaada wa China umewasili Sudan
Msaada uliotolewa na serikali ya China kwa Sudan Kusini kwa ajili ya kupambana na virusi vya Corona umewasili mjini Juba. Msaada huo ni pamoja na nguo za kujikinga, barakoa, miwani ya kujikinga, glavu na vitendanishi.
Balozi wa China nchini Sudan Kusni Bw. Hua Ning amesema, China inafuatilia sana hali ya maambukizi ya COVID-19 nchini Sudan Kusini na kupenda kuiunga mkono Sudan Kusini katika kazi za kuzuia kuenea kwa virusi vya Corona.
Naibu waziri wa mambo ya nje wa Sudan Kusini Bw. Mayen Dut Wol ameishukuru China na kusema imetoa msaada kabla ya Sudan Kusini kuripoti mtu wa kwanza kuambukizwa COVID-19. Amesema msaada kutoka kwa serikali na makampuni ya China utaendelea kutoa mchango muhimu katika mapambano dhidi ya virusi hivyo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |