Washukiwa wa Boko Haram wauawa Nigeria
Watu wasiopungua 81 wameuawa na wengine saba wametekwa nyara wakati watu wanaoshukiwa kuwa ni wapiganaji wa Boko Haram waliposhambulia kijiji kimoja katika jimbo la Borno, kaskazini mashariki mwa Nigeria.
Gavana wa jimbo la Borno Bw. Babagana Zulum amesema watu wengine 13 wamejeruhiwa na wapiganaji hao ambao walishambulia kijiji cha Faduma Koloram kwenye eneo la Gubio mapema Jumanne.
Gavana huyo amesema shambulizi hilo ni la tatu dhidi ya kijiji hicho ndani ya mwezi mmoja, na serikali itaendelea kuunga mkono vikosi vya usalama kuhakikisha usalama wa maisha na mali za watu wa huko.
Tukiwa bado Nigeria ni kwamba, Serikali ya taifa hilo imesema watu milioni 40 wa nchi hiyo wanakadiriwa kupoteza ajira zao kabla ya mwisho wa mwaka huu, kutokana na hatua za zuio na kudumisha umbali wa kijamii zilizochukuliwa kuzuia kuenea kwa COVID-19.
Makamu wa rais Yemi Osinbajo akinukuu takwimu za Shirika la Takwimu la Taifa NBS, amesema wanigeria milioni 39.4, ambao ni asilimia 33.6 ya jumla ya watu wa nchi hiyo, wanaweza kuathiriwa na janga hilo, na wengine wengi zaidi wanakadiriwa kuangukia katika ufakara kabla ya janga hilo kumalizika.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |