Ulaya yalaumiwa kwa mateso ya wahamiaji Libya
Shirika la kimataifa la utetezi wa haki za bindaadamu la Amnesty International limetupia lawama Umoja wa Ulaya kwa ukiukwaji haki za wakimbizi na wahamaji Libya.
Ripoti hii inaonyesha Uingereza ikikosoa Umoja wa Ulaya na mataifa wanachama wake, kwa kuinga mkono serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Libya (GNA) yenye makao yake mjini Tripoli na kitendo cha kuweka ulinzi katika eneo la pwani ya Libya kwa lengo la kuzuia wakimbizi na wahamiaji wasiingie Ulaya na hatimaye kuwarejesha Libya.
Kwa Mujibu wa ripoti hiyo ni kwmba pia, mateso yameongezeka kutokana na masharti ya kukabiliana na janga la la virusi vya corona.
Shirika la Amnesty limesema wamekuwa wakipelekwa katika vituo vya kuwahifadhi ambako wanawekwa kizuizini kiholela na bila ya ukomo jambo ambalo shirika hilo linaeleza kuwa si la kiutu.
Shirika hilo imesema Umoja wa Ulaya haijatoa shinikizo lolotea kwa serikali inayoungwa mkono na jumuiya ya kimataifa kuheshimi haki za wakimbizi na wahamiaji.
Tangu kuondolewa madarakani na kuuwawa kwa kiongozi wa muda mrefu wa Libya, 2011, Muammer Gaddafi, taifa hilo lenye utajiri wa mafuta limeingia katika machafuko na katika miaka ya hivi karibuni limekuwa uwanja wa mapigano kwa makundi hasimu.
Mataifa ya Ulaya yamekuwa katika majaribio ya kutafuta suluhisho la vurugu hizo, ambazo zimetoa nafasi kwa wanofanya biashara ya usafirishaji haramu wa watu.
Kwa miaka kadhaa Umoja wa Mataifa na makundi ya utetezi wa haki za binaadamu yamekuwa yakirejea kuonya kwamba wahamiaji nchini Libya wapo katika hatari ya mateso, unyanyaswaji wa kijinsia na usafirishaji haramu wa watu.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |