Marekani kutangaza kurejesha vikwazo vya Umoja wa Mataifa dhidi ya Iran
Muda mchache baada ya Marekani kutangaza kurejesha vikwazo vya Umoja wa Mataifa dhidi ya Iran, washirika wake muhimu duniani – Ufaransa, Uingereza na Ujerumani – wamejitenga nayo, wakisema haina uhalali huo.
Mataifa hayo kwenye migogoro mbali ya kidunia yamekuwa yakisimama nyuma ya Marekani, yametowa msimamo wa pamoja yakisema kuwa uamuzi huo wa Marekani hauna nguvu za kisheria.
Kauli kama hiyo ilitolewa pia na Urusi, hasimu mkubwa wa Marekani. "Hatua na vitendo vilivyo kinyume na sheria vya Marekani kimsingi haviwezi kuwa na athari ya kisheria kwa nchi nyengine," ilisema taarifa ya mambo ya nje ya Urusi.
Kwa upande wake, Iran imesema kuwa Marekani inakabiliwa na kushindwa kwenye hatua yake hiyo. Rais Hassan Rouhani amesema kupitia hotuba yake ni kwamba nchi yake kamwe haitopiga goti mbele ya Marekani na kwamba itaijibu Marekani kama inavyostahiki.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |