Virusi vya corona: Mkuu wa afya asifu mapambano ya Afrika dhidi ya Covid-19
kuu wa kituo cha Afrika cha kudhibiti na kuzuwia magonjwa (ECDC) ameyasifu mataifa ya Afrika kwa kuweza kukabiliana na kusambaa kwa virusi vya corona.
Afrika imeshuhudia maambukizi ya corona ya watu milioni 1.4, na vifo 34,000 tangu mwezi wa Machi.
Idadi hiyo ni ndogo sana kuliko ile ya mabara ya Ulaya, Asia na Amerika Kaskazini na Amerika Kusini, huku idadi ya maambukizi ikiendelea kupungua.
Uingiliaji kati wa awali ulikuwa na mchango mkubwa katika kukabiliana na kusambaa , John Nkengasong amekiambia kipindi cha BBC Newsday.
Bara lenye watu zaidi ya bilioni moja limekuwa na chini ya 5% ya maambukizi ya virusi vya corona kote duniani na 3.6% ya vifo.
Dkt. Nkengasong ameyaelezea kama "uongo" madai kwamba idadi ya watu walioambukizwa virusi na vifo katika bara la Afrika haikuripotiwa ipasavyo.
" Huenda hatukubaini visa vyote, sawa na maeneo mengine ya dunia...lakini hatuwaoni watu katika maeneo ya bara wakiugua na kufa mitaani au mazishi ya watu wengi yakiendelea ," Dkt Nkengasong amesema.
Mataifa yote ya Afrika yalianzisha misururu ya hatua za kukabiliana na virusi mara tu mtu wa kwanza aliporipotiwa kuwa na virusi mwezi Machi.
Katika nchi nyingi , ikiwa ni pamoja na Afrika Kusini, zilianzisha vipindi vya kukaa nyumbani, lakini nyingine kama vile Ethiopia zilichagua kuweka sheria kidogo.
Dkt. Nkengasong, hatahivyo, anasema sababu ya kuwa na idadi ndogo ya maambukizi ni "juhudi za pamoja za bara ", ambazo zililenga juu ya "kuongeza idadi ya watu wanaopimwa na kufuatilia watu waliokutana na waliopata maambukizi- (contact tracing) na la muhimu zaidi watu walivaa barakoa ".
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |