• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Septemba 26-Oktoba 2)

    (GMT+08:00) 2020-10-02 15:29:36
    Félicien Kabuga: Mahakama ya Ufaransa yaamuru mshukiwa wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda ashtakiwe Tanzania.

    Mahakama ya rufaa nchini Ufaransa imekubali kumpeleka mshukiwa wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda Felicein Kabuga kushtakiwa nchini Tanzania. Bwana Kabuga alikamatwa nyumbani kwake nje ya mji wa Paris baada ya miaka 26 kama mtoro.

    Takriban watu 800,000 waliuawa nchini Rwanda katika mauaji ya kimbari ya 1994. Bwana Kabuga anadaiwa kuyapatia makundi ya wapiganaji fedha alipokuwa mwenyekiti wa kitaifa wa hazina ya ulinzi ya kitaifa.

    Amekana madai yote hayo. Wakati wa kusikilizwa kwa kesi yake mwezi Mei, alielezea madai hayo kama ya uwongo. Kabuga anashtakiwa kwa kufadhili mauaji ya kimbari nchini Rwanda. Anadaiwa kuwasaidia wapiganaji wa kabila la Hutu ambao waliwaua takriban raia wa Tutsi 800,000 pamoja na Wahutu walio na msimamo wa kadri 1994.

    Alianzisha kituo cha habari cha redio Télévision Libre des Mille Collines (RTLM), ambacho kilidaiwa kutoa wito kwa watu kuwaua watu wa kabila la Tutsi. Mwaka 1997 alishtakiwa kwa mashtaka 7 ikiwemo mauaji ya kimbari na uhalifu dhidi ya binadamu na jopo la kimataifa lililokuwa likichunguza mauaji hayo.

    Maafisa wa polisi wanasema kwamba bwana Kabuga alitumia majina 28 tofauti kujificha. Akiwa mtoro , alidaiwa kuishi katika mataifa mbalimbali Afrika mashariki ikiwemo Kenya, ambapo yeye na familia yake walikua na biashara. Muendesha mashtaka wa Ufaransa alisema kwamba amekuwa akiishi kupitia utambulisho bandia.

    Je, Felicien Kabuga ni nani?

    Ndiye aliyekuwa mtu tajiri zaidi nchini Rwanda kabla ya mauaji ya 1994.

    Akijipatia utajiri wake kupita biashara ya majani ya chai mwaka 1970 na alifanya biashara katika sekta chungu nzima nyumbani na katika mataifa ya kigeni.

    Alikuwa mshirika wa karibu wa chama tawala cha MRND - na alikuwa na uhusiano na rais wa zamani Juvenal Habyarimana ambaye alifariki 1994.

    Akituhumiwa kwa kuwa mfadhili mkuu wa mauaji hayo na kutumia biashara yake na uwezo wake kupanga na kufadhili mauaji.

    Miezi kadhaa baada ya mauaji hayo , baraza la usalama la umoja wa mataifa lilianzisha mahakama ya mauaji ya kimbari nchini Rwanda mjini Arusha, kaskazini mwa Tanzania.

    Lengo lake ilikuwa kuwashtaki viongozi wa mauaji hayo na zaidi ya watu 60 walihukumiwa. Mahakama hiyo ilifungwa rasmi mwaka 2015 na baadaye utaratibu wa Mahakama za Kimataifa za Jinai MICT ulichukua usimamizi wake ili kuwasaka washukiwa wa mwisho.

    Mahakama hiyo haina maafisa wa polisi wala uwezo wa kukamata, na badala yake imekuwa ikitegemea serikali tofauti kuchukua hatua hizo badala yake.


    1  2  3  4  5  6  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako