Serikali ya Uganda imesema Jumanne kuwa itasaidia kufadhili miradi ya ujenzi wa zaidi ya kilomita 200 za barabara ndani ya DRC kama sehemu ya mipango ya kuboresha biashara kati ya mataifa hayo. Uganda itachangia karibu asilimia 20 ya thamani ya mradi huku kiasi kingine kikitolewa na serikali ya Congo katika mradi wa ushirikiano kati ya sekta ya umma na binafsi. Haya yamesemwa na waziri wa ujenzi na usafiri wa Uganda Jenerali Katumba Wamala.
Utaratibu kama huo sio wa kawaida katika eneo ambako serikali zinapambana kupanua mitandao ya barabara ndani ya mipaka yake. Licha ya ukubwa wake na utajiri wa rasilimali, Congo inasalia kuwa moja ya mataifa maskini zaidi duniani. Eneo la mashariki mwa nchi hiyo limegubikwa hasa na vurugu za makundi ya waasi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |