Makamu wa rais ambaye pia ni waziri mkuu wa Falme za Kiarabu na mtawala wa Dubai Mohammed bin Rashid Al Maktoum amekiri kupigwa chanjo ya COVID-19 iliyotengenezwa na China.
Habari zinasema kuwa, chanjo hiyo ilichunguzwa na kampuni ya Sinopharm, hivi sasa ipo kwenye kipindi cha tatu cha majaribio ya hospitalini. Vyombo vya habri vilinukuu habari kutoka serikali ya Falme za Kiarabu ikisema kuwa, chanjo hiyo ni salama na yenye ufanisi. Kabla ya Bw. Al Maktoum kupigwa chanjo hiyo, maofisa 10 wa nchi hiyo walipigwa chanjo hiyo. Aidha madaktari na wauguzi wa nchi hiyo pia watapigwa chanjo hiyo.
Habari nyingine zinasema, Bahrain imeidhinisha wafanyakazi wanaoshughulikia kudhibiti janga la COVID-19 wapigwe chanjo haraka yaCOVID-19 kutoka China kuanzia tarehe 3 mwezi Novemba.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |