Siku ya jumatano waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed alisema jeshi la Ethiopia limefanikiwa kudhibiti shambulio la waasi katika eneo la kaskazini la Tigray. Awali hofu ilitanda ya kutokea vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo, baada ya Ahmed kutuma wanajeshi wa kupambana na ghasia hizo za Chama cha Ukombozi wa Watu wa Tigray, TPLF kinachodhibiti eneo hilo. Serikali inadai wanachama wa chama cha TPLF waliishambulia kambi ya kijeshi huko Tigray. Aidha serikali imetangaza hali ya hatari kwa miezi sita katika eneo la Tigray, linalopakana na Eritrea. Umoja wa Mataifa umetoa wito wa kutuliza ghasia hizo, ukisema kwamba utulivu nchini Ethiopia ni muhimu kwa eneo zima la Pembe ya Afrika, ambalo linazijumuisha Somalia na Sudan.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |