Mshukiwa wa uhalifu wa kivita nchini Kosovo ambaye pia alikuwa msemaji wa zamani wa kundi la uasi la Kialbania, Jakup Krasniqi, amekamatwa mjini Pristina na kufikishwa katika mahakama ya (KSC) ya huko The Hague, iliyoundwa kuchunguza uhalifu wa kivita wakati wa mzozo wa Kosovo miaka ya 1990.Taarifa iliyotolewa na mahakama hiyo imesema, Krasniqi atakabiliwa na mashtaka yanayohusiana na uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu. Krasniqi alikuwa msemaji wa Jeshi la Ukombozi wa Kosovo (KLA), wakati wa mzozo wa 1998-9 ambao mwishowe uliishia kupatikana uhuru wa Kosovo kutoka Serbia miaka 10 baadaye. Krasniqi alikamatwa baada ya polisi wa Umoja wa Ulaya waliokuwa na silaha, kuivamia nyumba yake na kufanya upekuzi kwa saa kadhaa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |