Rais Uhuru Kenyatta, naibu wake William Ruto, Kinara wa ODM, Raila Odinga na viongozi wa vyama vingine vikuu nchini Kenya wameshauriwa kushiriki mazungumzo kutafuta mwafaka kuhusiana na utata unaozingira Mpango wa Upatanishi BBI.
Wazee wa Jamii za Kenya wanadai kuwa hapana haja ya viongozi kuwa na misimamo tofauti kuhusu BBI, hali ambayo ikalazimu kura ya maoni kufanyika nchini.
Wameongeza kuwa iwapo kura ya maoni itaandaliwa huenda ikachochea uhasama miongoni mwa jamii mbali mbali na kusababisha machafuko.
Aidha wamesisitiza kuwa fedha ambazo zinapendekezwa kuandaa kura ya maoni ni nyingi na zinaweza kutumika kuwasaidia wakenya ambao wanapitia hali ngumu ya maisha.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |