China na Ufaransa zina msimamo wa thamani wa pamoja katika maoni ya usimamizi wa ulimwengu
2019-03-26 19:20:14| CRI

Ujenzi wa barabara kuu namba 1 inayounganisha Brazzaville, mji mkuu wa Jamhuri ya Kongo na kituo kikuu cha uchumi Pointe-Noire ulikamilika mwaka 2016, na ulipunguza muda wa safari kati ya miji hiyo miwili kutoka wiki moja hadi saa 6. Barabara kuu hiyo ilijengwa na kampuni ya CSCEC ya China na kusimamiwa na kampuni ya EGIS ya Ufaransa. Baada ya kujengwa kwa barabara kuu hiyo, China na Ufaransa zimeshirikiana tena, China ikiwajibika na ukarabati wa uendeshaji wa barabara na Ufaransa ikishughulikia usimamizi wa uendeshaji huo.

Barabara kuu hiyo ni mfano wa kuigwa ambao China na Ufaransa zinashirikiana kuendeleza soko la upande wa tatu. Nchi hizo mbili ambazo ni nchi wajumbe wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na nguvu muhimu za kiuchumi duniani, kutokana na maoni mengi yanayofanana kuhusu thamani, zina msingi imara na mustakabali mkubwa wa ushirikiano katika ajenda nyingi za usimamizi wa ulimwengu. Kati ya maoni hayo yanayofanana, muhimu zaidi ni kwamba pande zote mbili ni watendaji halisi wa kulinda mfumo wa pande nyingi.

Rais Xi Jinping wa China amesema, hatua za upande mmoja na ulinzi wa kibiashara unaongezeka na kuharibu utaratibu wa kimataifa na utaratibu wa usimamizi wa ulimwengu, dunia inahitaji zaidi mfumo wa pande nyingi. Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa pia anaona kuwa mfumo wa pande nyingi ni njia nzuri zaidi ya kukabiliana na changamoto za dunia.

Katika usimamizi wa ulimwengu unaokabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa, Ufaransa imetoa mchango mkubwa wa kuhimiza kazi hiyo, na uungaji mkono wa China pia ni muhimu sana. Wachambuzi wanasema, kufuatia Marekani kujitoa kutoka makubaliano ya Paris, kama China ikichagua kujitoa kutoka makubaliano hayo kutokana na maendeleo ya uchumi wake, makubaliano ya Paris hayataweza kutekelezwa.

China ni nchi inayonufaishwa na kuchangia mafungamano ya kiuchumi ya dunia, na rais Xi Jinping wa China ametoa pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja" kwa dunia nzima, hivi sasa nchi na mashirika zaidi ya 150 yamejiunga na pendekezo hilo. Rais Macron mwaka jana pia ametangaza kuwa Ufaransa itajiunga na pendekezo hilo, huku akisema kuwa pendekezo hilo ni la kunufaishana.

Uhusiano kati ya China na Ufaransa ni wa kimkakati, hivyo ushirikiano kati ya nchi hizo mbili utatoa mchango muhimu katika kulinda utaratibu wa ulimwengu.