China yatoa mapendekezo kwa ufumbuzi wa matatizo makuu yanayokabili usimamizi wa mambo ya dunia
2019-03-27 17:09:10| CRI

Sherehe ya kufungwa kwa Baraza la usimamizi wa mambo ya dunia kati ya China na Ufaransa ilifanyika jana huko Paris, rais Xi Jinping wa China alitoa hotuba kuhusu "kuchangia busara na nguvu katika kuijenga dunia iwe nzuri zaidi", akitoa mapendekezo ya China kuhusu ufumbuzi wa matatizo makuu yanayokabili usimamizi wa mambo ya dunia, na kuzitaka nchi mbalimbali kuchukua hatua halisi katika mambo hayo, na kufanya juhudi za pamoja ili kutimiza kujiamulia mustakabali kwa binadamu.

Hivi sasa dunia inakabiliwa na mabadiliko makubwa ambayo hayakutokea katika miaka mia moja iliyopita, wakati masoko mapya ya kiuchumi na nchi zinazoendelea zinapata maendeleo makubwa, huku duru mpya ya mapinduzi ya sayansi na teknolojia na mageuzi ya viwanda ikihimiza aina mpya ya viwanda, na kuingiza msukumo mpya katika mabadiliko ya msukumo wa zamani na mpya, na mchakato wa mafungamano ya kiuchumi duniani. Wakati huo huo, utaratibu wa upande mmoja na vitendo vya kujilinda kibiashara vinavyoongezeka kwa udhahiri, vimeharibu vibaya utaratibu na biashara ya pande nyingi, ugaidi, migogoro ya wakimbizi, mabadiliko ya hali ya hewa pia vinazidi kuenea, na kuleta wasiwasi mkubwa zaidi wa hali ya kutokuwa na utulivu na kutotabirika, inayomkabili binadamu.

Rais Xi Jinping wa China akiwa kiongozi wa nchi ya pili kwa nguvu ya kiuchumi duniani, na nchi kubwa zaidi inayoendelea, amefikiria kwa makini na kwa muda mrefu kuhusu maendeleo ya mabadiliko ya utaratibu wa kimataifa, na kutoa mapendekezo matano, nayo ni pamoja njia muhimu katika kushughulikia mapungufu katika usimamizi wa mambo ya dunia ambayo ni kushikilia mtizamo wa usimamizi wa mambo ya dunia unaofuata kanuni za kujadiliana, kujenga kwa pamoja na kunufaika kwa pamoja; njia muhimu ya kutafuta ufumbuzi wa upungufu wa imani ni kutafuta maslahi ya pamoja huku tukiheshimu uwepo wa maoni tofauti, na kuongeza kuaminiana kimkakati kwa mazungumzo na kupunguza kutiliana shaka; njia muhimu ya ufumbuzi wa upungufu wa amani ni kufuata mtizamo mpya wa usalama ulio wa pamoja, shirikishi, ushirikiano na wa kudumu; na kipaumbele cha ufumbuzi wa upungufu wa maendeleo ni kushikilia kufanya uvumbuzi, kuchukua hatua kwa pamoja, kuwa na usawa na kusikilizana, ili kuongoza mchakato wa mafungamano ya kiuchumi kupata maendeleo zaidi.

Hotuba hiyo ya rais Xi imepata uungaji mkono wa viongozi wa Ulaya waliohudhuria sherehe ya kufungwa kwa Baraza la usimamizi wa mambo ya dunia kati ya China na Ufaransa. Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa amesema kwenye mtandao wa kijamii kwamba, "Umoja wa Ulaya na China zitashirikiana katika kukabiliana kwa pamoja changamoto zinazoikabili dunia nzima". Mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Ulaya Bw. Jean Claude Juncker amesema pande zote mbili za Umoja wa Ulaya na China zina nia ya kujenga uhusiano wa karibu wa ushirikiano na wa kiwenzi. Naye chansela wa Ujerumani Bibi Angela Merkel amependekeza kufanyika kwa mazungumzo kati ya viongozi wa Ulaya na China. Mapendekezo hayo ya ufumbuzi yanayoonesha busara ya wachina, ni chaguo lenye busara kwa watu wanaochukulia mambo ya dunia, China na nchi zao kwa mtizamo sahihi.