Hainan yashuhudia tena China kuzidi kufungua mlango wake
2019-03-28 19:45:30| CRI

Katika mkutano wa baraza la Boao la Asia uliofanyika mwaka jana mkoani Hainan, rais Xi Jinping wa China alitangaza kuzidi kulegeza masharti ya soko, kujenga mazingira ya uwekezaji yenye mvuto mkubwa zaidi, kuimarisha ulinzi wa hakimiliki ya ujuzi, kuzidi kuongeza manunuzi ya bidhaa kutoka nje, na kuanzisha duru mpya ya ufunguaji mlango zaidi ya China. Baada ya mwaka mmoja, katika mkutano wa mwaka wa baraza hilo, waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang ametoa tena ishara za kufungua mlango zaidi. Hainan ambayo ni dirisha muhimu la sera za ufunguaji mlango na mageuzi katika miaka 40 iliyopita, imeshuhudia tena China kuzidi kufungua mlango wake.

Katika ufunguzi wa mkutano wa baraza la Boao la Asia, waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang ametoa ishara ya ufunguaji mlango wazi inayosisimua. Hatua halisi ni pamoja na serikali ya China inataka kumaliza sheria zinazoendana na sheria ya uwekezaji wa kigeni kabla ya mwisho wa mwaka huu, kutekeleza kwa pande zote "mashirika ya kigeni kupigwa marufuku ama kuruhusiwa kuingia nchini China", kuhimiza kufungua soko la hisa, kuongeza fidia inayowekwa na sheria ya hakimiliki ya ujuzi, kutoruhusu kulazimisha kukabidhi teknolojia na kuboresha mfumo wa malalamiko ya mashirika ya kigeni.

Hatua hizo zinahusiana na sekta mbalimbali ikiwemo mashirika ya kigeni kuingia katika soko la China, mazingira ya uwekezaji, ulinzi wa hakimiliki ya ujuzi na ushirikiano wa teknolojia. Hatua hizo sio tu ni kipaumbele cha duru mpya ya ufunguaji mlango ya China, bali pia ni ufuatiliaji mkubwa wa uwekezaji wa kigeni kuendelea nchini China. Kujibu masuala hayo na kuchukua hatua halisi ni mahitaji ya China kuzidi kufungua mlango, na pia inaisaidia dunia kutumia fursa ya China na kuonesha majukumu yaliyotekelezwa na China kwa maendeleo ya dunia.

Akizungumzia uzoefu wa sera ya ufunguaji mlango wazi na mageuzi ya China, Rais Xi amesema, China inatakiwa kushikilia kuzidi kufungua na kuendelea kujenga kwa pamoja jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja. Kaulimbiu ya mkutano huo ni "Hatma ya pamoja, Hatua za pamoja, Maendeleo ya pamoja," ufunguaji mlango umekuwa neno kuu la mkutano huo, na umekuwa maoni ya pamoja na matarajio ya dunia.