Viongozi wa China na Ulaya wakubaliana kupanua maslahi ya pamoja na mafanikio ya kunufaishana
2019-04-10 16:49:06| CRI

Viongozi wa China na Ulaya wakubaliana kupanua maslahi ya pamoja na mafanikio ya kunufaishana

Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang ameanza ziara yake katika nchi za Ulaya, ikiwa ni baada ya rais Xi Jinping kufanya ziara ya kwanza katika nchi tatu za Ulaya mwaka huu, hatua ambayo imeonesha umuhimu wa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Ulaya.

Waziri mkuu Li ameshiriki kwenye mazungumzo ya 21 ya viongozi wa China na Umoja wa Ulaya huko Brussels, Ubelgiji, kwa pamoja na mwenyekiti wa Baraza la Ulaya Bw. Donald Tusk, na mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Ulaya Bw. Jean-Claude Juncker, na kutoa taarifa ya pamoja. Mazungumzo hayo ni utaratibu wa ngazi ya juu zaidi wa mazungumzo ya kisiasa kati ya China na Ulaya, na pande hizo mbili zilisherehekea kwa pamoja Maadhimisho ya miaka 20 tangu utaratibu huo uanzishwe.

Mazungumzo ya mwaka huu ni mwanzo mpya wa uhusiano kati ya pande hizo mbili. Kwenye mazungumzo hayo, pande hizo mbili zimekubailiana kushirikiana kupanua maslahi ya pamoja, na kuendelea kuimarisha mafanikio ya kunufaishana. Viongozi wa pande hizo mbili wamefikia makubaliano muhimu katika kulinda utaratibu wa pande nyingi na biashara huria, kuimarisha ushirikiano katika uvumbuzi wa sayansi na teknolojia, kusukuma mbele mazungumzo kuhusu makubaliano ya uwekezaji kati ya China na Ulaya, kupanua masoko kati ya pande mbili, na kuimarisha maingiliano. China na Ulaya, zikiwa ni nguvu mbili muhimu katika kulinda amani, ustawi na maendeleo ya dunia, ni muhimu kwa pande hizo mbili kuratibu sera na hatua katika mchakato wa kutafuta amani na maendeleo, ustawi wa pamoja na kuhimiza usimamizi wa dunia. Hivi sasa ushirikiano wenye ufanisi kati ya pande hizo mbili umezidi kuimarishwa na kupata mafanikio halisi na kuwanufaisha watu wa pande zote mbili. Chansela wa Ujerumani Bibi Angela Merkel ameeleza kwenye Mkutano wa viongozi wa Umoja wa Ulaya uliofanyika mwezi Machi kuwa, Ujerumani itachangia katika pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja, na kutaka kupata mafanikio ya kunufaishana. Gazeti la Handelsblatt la Ujerumani pia limeeleza kuwa, pendekezo hilo limetoa fursa za kihistoria kwa Ulaya na kuleta faida kubwa.

China na Ulaya ni wenzi wa kuwajibika wa upande mwingine, na msukumo muhimu wa kuhimiza amani, utulivu na ustawi wa dunia. Kuzidi kuimarisha uhusiano wa kiwenzi na kimkakati kwa pande zote kati ya pande hizo mbili, kukuza ufunguaji mlango na ushirikiano, kuongeza faida ya kunufaishana, kujenga kwa pamoja uchumi wa dunia ulio wazi, kuhimiza kwa pamoja usimamizi wa dunia, si kama tu kutawanufaisha watu wa pande hizo mbili, bali kutaingiza utulivu na uhai mpya kwa utaratibu wa dunia.