China kuendelea kuwa msukumo muhimu wa kuhimiza ongezeko la uchumi duniani
2019-04-11 17:35:48| CRI

Idara ya Takwimu ya China imesema, mwezi Machi faharisi ya bei za walaji ya China yaani CPI cha China kimepungua kwa asilimia 0.4, ikiwa ni ongezeko la asilimia 2.3 kuliko mwaka jana wakati kama huu, huku kiashiria cha uzalishaji PPI kikiongezeka kwa asilimia 0.1, ikiwa ni ongezeko la asilimia 0.4. Kabla ya hapo, Shirika la Fedha Duniani IMF lilipandisha makadirio ya ongezeko la uchumi la mwaka 2019 hadi asilimia 6.3, ambalo linaongezeka kwa asilimia 0.1 kuliko makadirio ya mwezi Oktoba. China imekuwa nchi pekee ambayo makadirio ya ongezeko la uchumi yamepandishwa kati ya makundi matano muhimu ya uchumi duniani.

Matokeo hayo hayakupatikana kwa urahisi. Tokea mwaka jana, China imechukua hatua mbalimbali za kukuza mageuzi na kufungua mlango zaidi. Takwimu zimeonesha kuwa, mwaka 2018 matumizi ya mitaji ya kigeni ya China yalifikia dola za kimarekani bilioni 134.97, ikiwa ni ongezeko la asilimia 3, na kuweka rekodi mpya katika historia, huku uwekezaji wa moja kwa moja katika nchi za nje ukifikia dola za kimarekani bilioni 130, na kushika nafasi za kwanza duniani. Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Apple Bw. Tim Cook amesema, ufunguaji mlango wa China una umuhimu mkubwa katika kuhimiza usitawi wa dunia.

Kwa mujibu wa makadirio mapya yaliyotolewa na IMF, ongezeko la uchumi wa China linakadiriwa kufikia asilimia 6.3, ambalo limefikia lengo la ongezeko la makadirio hayo lililowekwa na serikali likiwa kati ya asilimia 6 na 6.5. Kama naibu meneja mkuu wa IMF Bw. Zhang Tao alivyosema, endapo China itatimiza ongezeko la uchumi la asilimia 6.3 mwaka huu, uchumi wa China utaweka rekodi mpya zaidi katika historia. Kwa upande mwingine, asilimia 6.3 kikiwa kiwango cha juu zaidi kinachowekwa na IMF kwa makundi makubwa ya kiuchumi duniani, hali inayoonesha kuwa, China, ambayo maendeleo yake yamebadilika na kuwa na sifa bora zaidi, itaendelea kuongoza makundi makubwa matano ya kiuchumi duniani, na kuwa msukumo mkubwa wa kuhimiza ongezeko la uchumi duniani.

Lakini hivi sasa binadamu bado anakabiliwa na mabadiliko makubwa ambayo hayawahi kutokea katika miaka 100 iliyopita, na kukabiliana na fursa za duru jipya ya mapinduzi na mageuzi ya viwanda, pamoja na hatari na changamoto kutokana na hali ya kujilinda kibiashara na utaratibu wa upande mmoja. Kutokana na hali hii, kufufuka kwa uchumi wa dunia kunatakiwa kutegemea uratibu na ushirikiano kati ya makundi mbalimbali ya kiuchumi. Kama Ripoti ya Makadirio ya uchumi wa Dunia iliyotolewa na IMF, makundi mbalimbali ya kiuchumi yanahitaji kuchukua sera za kuhamasisha uchumi kwa kulingana na hali ilivyo ya nchi, kuimarisha matokeo ya sera hizo, kutatua haraka iwezekanavyo migogoro ya biashara, ili kuongeza imani ya wawekezaji na wateja.