Rais Xi Jinping wa China aandika barua ya kujibu wanafunzi wa sekondari ya juu wa Marekani
2019-04-22 19:35:17| CRI

Kuhusu Rais Xi Jinping wa China kuandika barua kwa kujibu wanafunzi wa sekondari ya juu wa Marekani, msemaji wa wizara ya mambo ya nje Bw. Geng Shuang amesema hii si mara ya kwanza kwa rais Xi kuandika barua kwa wanafunzi wa nchi za nje, ambayo inaonyesha kufuatilia kwake ushirikiano wa mawasiliano wa China na nchi za nje.

Bw. Geng ameongeza kuwa wanafunzi hao zaidi ya 40 wanaosoma kwenye sekondari ya juu ya Niles Kaskazini ya jimbo la Illinois na kujifunza lugha ya Kichina kwa muhula mmoja tu, waliandika barua kwa Kichina na kuuliza maswali mengi, na rais Xi amejibu maswali hayo kuhusu hali yake ya kazi, maisha na tabia, na kuwahimiza wanafunzi hao kujitahidi kujifunza Kichina na kuongeza kutoa mchango kwa urafiki kati ya China na Marekani, na kuwakaribisha watembelee China.

Hii ni barua ya kuhimiza mawasiliano ya watu kati ya China na Marekani. Msingi wa mawasiliano ya nchi ni mawasiliano na maelewano ya watu, na lengo la mwisho la mawasiliano hayo ni kuwanufaisha watu wao. Kama mawasiliano kati ya watu yatafanywa kwa nia imara na kwa kina, yanaweza kuwa msingi wa kiraia wa kuihimiza serikali kuchukua sera za kirafiki na kuhakikisha mwelekeo unakuwa wa utulivu na maendeleo ya uhusiano kati ya nchi kutobadilika.

Katika miaka 40 iliyopita tangu China na Marekani zianzishe uhusiano wa kibalozi, pande hizo mbili zimefanya mawasiliano mengi katika sekta za elimu, sayansi na teknolojia, utamaduni, afya na michezo, ambayo yametoa mchango katika kuhimiza na kuboresha maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

Rais Xi aliwahi kusisitiza kuwa mawasiliano ya utamaduni na watu ni msingi wa uhusiano kati ya China na Marekani, huku akiwataka vijana kurithi shughuli za kirafiki za nchi hizo mbili. Wakati akiwa ziarani nchini Marekani, rais Xi alitembelea shule ya sekondari ya huko na kuwaalika wanafunzi wa Marekani kutembelea China. Katika barua hiyo, rais Xi pia amesema kuwa vijana ni siku za mbele za urafiki kati ya China na Marekani, huku akitilia maanani katika siku za mbele za kati ya nchi hizo mbili na maslahi kwa watu wa pande mbili.

Wakati dunia inakabiliwa na mabadiliko makubwa ambayo hayajawahi kutokea katika miaka mia moja iliyopita, migongano na mikwaruzano kati ya China na Marekani inaongezeka, huku uhusiano kati ya nchi hizo mbili ukibadilika na kurekebishwa kwa kina. Wachina wanaoendelea kufungua mlango wanazidi kuielewa Marekani, lakini wamarekani wengi bado wanapata taswira ya China kupitia vyombo vya habari vya Marekani vyenye upendeleo. Hivyo mawasiliano hayo yanatakiwa kuongezeka badala ya kufunga mlango, au kuzuia mawasiliano hayo. Kuhimiza mawasiliano katika sekta mbalimbali hasa mawasiliano kati ya vijana kutakuwa nguvu kuu ya kuondoa migongano kati ya nchi hizo mbili, kutimiza ushirikiano wa kunufaishana na kutekeleza kwa pamoja majukumu ya dunia nzima.