Jeshi la majini la China kuendelea kufanya juhudi kujenga jumuiya ya bahari yenye mustakabali wa pamoja
2019-04-23 20:04:38| CRI

Shughuli za maadhimisho ya miaka 70 ya jeshi la majini la China zimefanyika huko Qingdao,China Rais Xi Jinping wa China amekutana na viongozi wa ujumbe wa majeshi ya majini ya nchi mbalimbali, huku akikagua kundi la manowari na kundi la ndege la jeshi la majini la China, na kundi la manowari la majeshi ya majini ya nchi mbalimbali yanayoshiriki kwenye shughuli hizo. Rais Xi pia kwa mara ya kwanza ametoa pendekezo la kujenga jumuiya ya bahari yenye mustakabali wa pamoja, ambalo limeweka bayana mwelekeo wa maendeleo ya jeshi la majini la China, na kuhimiza mawasiliano kati ya China na nchi za nje kwenye bahari na ushirikiano katika sekta mbalimbali.

Baada ya maendeleo ya miaka 70, jeshi la majini la China hivi sasa limekuwa na nguvu ya baharini inayoweza kufanya mashambulizi ya kawaida na ya kinyuklia, kufanya tishio au shambulizi halisi chini ya mazingira ya mtandao wa internet na kutekeleza operesheni mbalimbali za kijeshi. Ukaguzi huo umeonesha kwa ujumla mafanikio ya ujenzi wa kisasa wa jeshi la majini la China na kufungua mlango kwenye kiwango cha juu na kuoneshaimani iliyonalo jeshi hilo.Ukaguzi wa jeshi la majini la China huko Qingdao umekuwa sherehe kubwa ya diplomasia ya kijeshi ya China. Manowari karibu 20 kutoka nchi zaidi ya kumi ikiwemo Russia, Thailand, Vietnam, India zimeshiriki kwenye shughuli hiyo. Ushiriki wa majeshi ya majini ya nchi mbalimbali umeonesha nia za nchi kulinda amani kwa pamoja na kutafuta maendeleo kwa pamoja.

Hivi leo mazingira ya maendeleo ya usalama wa bahari ya China yanakabiliwa na changamoto na fursa kubwa. Hasa utoaji wa pendekezo la "Njia Hariri ya Baharini ya Karne 21" umetoa jukwaa jipya kwa China kuhimiza maendeleo ya uchumi wa bahari na mafungano ya utamaduni wa bahari. Jeshi la majini la China likiwa nguvu kuu ya baharini ya taifa, linatakiwa kubeba majukumu mapya.

Rais Xi alipokutana na ujumbe wa majeshi ya majini ya nchi za nje amesisitiza, ulimwengu huo wa rangi ya buluu ambao binadamu wanaishi, umeunganishwa kwa bahari kuwa jumuiya yenye mustkabali wa pamoja. Katika siku za baadaye, jeshi hilo litafanya juhudi pamoja na majeshi ya majini ya nchi mbalimbali duniani kulinda amani na usalama wa bahari, kuhimiza maendeleo na ustawishaji wa bahari na kuendelea kutoa mchango katika ujenzi wa jumuiya ya bahari yenye mustakbali wa pamoja.