Idara ya safari ya anga ya juu ya China yatoa fursa ya ushirikiano kwa jumuiya ya kimataifa
2019-04-24 19:53:34| CRI

Leo ni siku ya nne ya safari za anga ya juu ya China, habari nyingi za kusisimua zimetolewa: China imetangaza maendeleo mapya ya utafiti wa kituo cha anga ya juu na imefanikiwa kurusha vyombo 12 vya safari za anga ya juu, chombo cha anga ya juu Tiangong-1 na maabara ya Tiangong-2, huku ikituma wanaanga 11 kwenye anga ya juu na kuwarejesha salama; satelaiti ya 44 ya Beidou hivi karibuni imerushwa katika anga ya juu na kuzindua uundaji wa mtandao wa satelaiti za Beidou kwa mwaka 2019; hasa katika operesheni ya uchunguzi wa mwezi ya Chang'e 6 itakayotekelezwa, na operesheni ya kurejesha sampuli kutoka kwenye sayari ndogo, China pia itatoa fursa ya ushirikiano kwa jumuiya ya kimataifa.

Idara hiyo imetoa taarifa ikisema, mradi wa kubeba vifaa utafanywa kwenye chombo cha uchunguzi cha Chang'e 6. Kabla ya hapo, Machi 25 China na Ufaransa zilisaini makubaliano ya mpango wa kuchunguza mwezi, na Ufaransa itaweka vifaa vya majaribio vyenye uzito wa kilo 15 kwenye chombo hicho ikiwemo kamera moja na kifaa cha utafiti.

Katika opereshereni nyingine ya kuchunguza sayari ndogo iliyoko karibu na dunia 2016HO3, China itakusanya mapendekezo ya miradi ya kubeba vifaa kote duniani kwa kufuata kanuni za kukusanya mitaji, kubeba bila malipo na kutumia data kwa pamoja.