Mkutano wa pili wa kilele wa ushirikiano wa kimataifa wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja" utakaofanyika kwa siku tatu umefunguliwa leo hapa Beijing, na wajumbe 5,000 hivi kutoka nchi zaidi ya 150 na mashirika zaidi ya 90 ya kimataifa wamehudhuria mkutano huo. Baada ya maendeleo ya kasi ya miaka miwili, ujenzi wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja" umekuwa jukwaa kubwa zaidi la kiuchumi na pendekezo la umma linalopendwa zaidi na pande nyingi lililotolewa na China kwa dunia nzima.
Tangu mwaka 2013 rais Xi Jinping wa China atoe pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja", ujenzi wa pendekezo hilo umepata mafanikio mengi, hasa baada ya China kufanya mkutano wa kwanza wa kilele wa Ukanda Mmoja na Njia Moja mwaka 2017, idadi ya nchi zinazoshiriki kwenye pendekezo hilo imeongezeka maradufu, huku miradi mbalimbali ya ujenzi ikitekelezwa kote duniani.
Bila shaka mkutano wa pili wa kilele wa ushirikiano wa kimataifa wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja" utakuwa shughuli nyingine muhimu ya kuhimiza dunia nzima kujadili kuhusu maendeleo ya sifa ya juu ya ujenzi wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja". Hivi karibuni, mjumbe wa taifa wa China ambaye pia ni waziri wa mambo ya nje Bw. Wang Yi amesema, maendeleo ya sifa ya juu ni wazo la kimsingi, wala si kigezo rahisi. China inapendekeza kuwa ujenzi wa pamoja wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja " unatakiwa kufuata vigezo na kanuni za kimataifa zinazokubaliwa na jumuiya ya kimataifa, na kulingana na utekelezaji bora wa kimataifa wa maendeleo endelevu, ili kufanya kijani na ulinzi wa mazingira kuwa rangi ya msingi, utawala bora na ufanisi wa juu kuwa njia ya lazima, ufunguaji mlango na uvumilivu kuwa wazo la pamoja.
Katika miaka sita iliyopita tangu China itoe pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja", pendekezo hilo limeonesha mwelekeo mzuri wa ushirikiano wa pande mbili, tatu na nyingi. Ingawa baadhi ya nchi zilizoendelea hazijasaini makubaliano ya pendekezo hilo na China, lakini zimetoa huduma za ushauri, sheria na fedha kwenye miradi ya "Ukanda Mmoja na Njia Moja", hata kushiriki moja kwa moja kwenye ujenzi wa miradi hiyo, na kuwa nchi shirikishi za pendekezo hilo. Ushirikiano huo umeinua vigezo na kiwango cha ujenzi wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja", ambao pia umeweka msingi imara wa kujenga uhusiano mzuri zaidi wa kiwenzi katika siku za baadaye.
Kutokana na ushawishi wa pendekezo hilo, wakati baadhi ya mashirika ya kikanda yakihimiza mipango ya maendeleo, yameanza kuunganisha mipango yao na pendekezo hilo, kama vile ajenda ya mwaka 2063 iliyotolewa na Umoja wa Afrika, Mpango wa unganishaji wa Ulaya na Asia uliotolewa na Umoja wa Ulaya.
Rais Xi Jinping wa China amesisitiza kwa mara nyingi kuwa chimbuko la "Ukanda Mmoja na Njia Moja" liko nchini China, lakini pendekezo hilo linamilikiwa na dunia nzima. Wakati mkutano wa pili wa kilele wa ushirikiano wa kimataifa wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja" ukifanyika, watu wanaweza kutarajia kuwa "Ukanda Mmoja na Njia Moja" utaleta nafasi kubwa zaidi ya maendeleo kwa nchi mbalimbali duniani.