China inafungua mambo ya fedha kwa mpango wake mwenyewe
2019-05-03 11:31:37| CRI

Mwenyekiti wa Tume ya Kusimamia Benki na Bima nchini China Guo Shuqing amesema hivi karibuni China itatangaza hatua mpya 12 zinazolenga kufungua zaidi sekta ya benki na bima kwa nchi za nje.

Hii ni raundi ya pili kwa China kufungua sekta ya benki na bima baada ya hatua 15 za kufungua sekta hiyo zilizotangazwa mwezi Aprili mwaka jana kutekelezwa. Bila shaka, itainua kiwango cha ufunguaji mlango na nguvu ya soko kwa sekta hiyo, kukamilisha mazingira ya kibiashara katika mambo ya fedha, kuhamasisha makampuni ya nje kushiriki kwenye maendeleo ya mambo ya fedha ya China, na kuboresha huduma za mambo ya fedha nchini China katika mitazamo ya ushindani, soko, ubunifu na huduma.

Sekta ya fedha ni chombo cha kutuliza na nguvu ya kukuza maendeleo ya uchumi wa nchi. Watu wanaofuatilia uchumi wa China wanapaswa kugundua kuwa baada ya mkutano mkuu wa 19 wa Chama cha Kikomunisti cha China kuamua kufungua mlango kwa pande zote, mwaka jana katika mkutano wa mwaka wa Baraza la Asia la Bo'ao rais Xi Jinping wa China alitangaza hatua nne za kufungua mlango katika mambo ikiwemo fedha, mwaka huu ripoti ya utendaji kazi ya serikali ya China pia imetangaza kutekeleza ipasavyo hatua za kufungua mlango. Ufunguaji wa sekta ya fedha unatekelezwa kwa mkakati uliopangwa nchini China.

Safari hii China itatoa hatua hizi mpya 12 kwa ajili ya kutekeleza kwa undani mpangilio wa kufungua sekta ya fedha ya China, hii inalingana na mahitaji ya maendeleo ya uchumi na mambo ya fedha. Kwa mujibu wa maudhui yake, hatua hizo 12 zina sifa kuu tatu, moja ni kusisitiza kanuni ya vigezo sawa kwa makampuni ya ndani na ya nje; pili ni kupunguza masharti ya mashirika ya fedha ya nchi za nje kuingia katika soko la China; tatu ni kupanua wigo wa biashara ya mashirika hayo ya kigeni.

Sekta ya fedha imepata maendeleo makubwa katika miaka 40 iliyopita tangu China ianze kutekeleza sera ya mageuzi na kufungua mlango . Lakini hali halisi ni kuwa kiwango cha maendeleo na ufunguaji cha sekta ya fedha ya China bado hakilingani na hadhi ya uchumi wa China inayoshika nafasi ya pili kiuchumi duniani, ndio maana bado kuna nafasi kubwa za kufungua sekta hiyo.

Hivi karibuni, rais Xi Jinping wa China alitangaza hatua tano za kufungua zaidi mlango kwenye kongamano la ngazi ya juu la ushirikiano wa kimataifa la "Ukanda Mmoja, Njia Moja", mojawapo ikiwa ni kupunguza masharti ya makampuni ya kigeni kuingia katika soko la China.

Sekta ya fedha kimsingi ni sekta ya huduma yenye ushindani, na kwa kupitia kufungua mlango na kushiriki kwenye ushindani wa masoko ya kimataifa, inaweza kuhudumia zaidi uchumi halisi. Hii ni fursa ya kihistoria kwa mashirika ya fedha ya China, na pia ni fursa kwa mashirika ya fedha ya kigeni ambayo yameingia au yataingia katika soko la China.