Je, New Zealand itakuwa kituo kinachounganisha Latin Amerika na China?
2019-05-07 21:03:53| CRI

Takwimu mpya zimeonesha kuwa mwezi wa Machi, thamani ya jumla ya mauzo ya bidhaa kwa nje ya New Zealand imefikia dola bilioni 3.76 za kimarekani na kuweka rekodi ya juu zaidi. Idara ya takwimu ya nchi hiyo imesema, rekodi hiyo inategemea ongezeko la mauzo ya bidhaa zake kwa China. Ukweli ni kwamba katika miaka ya hivi karibuni China imeipita Australia na kuwa mwenzi mkubwa zaidi wa biashara wa New Zealand. Thamani ya biashara za pande mbili kati ya China na New Zealand imezidi dola bilioni 19.8 za kimarekani.

Kwa ujumla sera ya New Zealand kwa China ni yenye busara na ufanisi. Nchi hiyo ilikuwa nchi ya kwanza ya magharibi iliyosaini makubaliano ya biashara huria na China, na pia ni nchi ya kwanza iliyoendelea iliyokuwa nchi mwanachama wa kuzindua Benki ya AIIB inayoongozwa na China. Mbali na hayo, New Zealand pia imejiunga mapema na pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja".

Hivi karibuni katika mkutano wa kilele wa biashara wa China mwaka 2019 uliofanyika nchini New Zealand, waziri wa ongezeko la biashara na mauzo ya bidhaa wa nchi hiyo Bw. David Parker, alisema pande mbili zina mustakabali mkubwa wa kufikia ushirikiano wa kunufaishana katika ujenzi wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja", kuinua uwazi au uvumbuzi wa mfumo. Hivi sasa New Zealand na nchi nyingine tano ikiwemo Russia zinafanya ushirikiano kufanya uratibu wa kuweka vigezo vya uhasibu vya nchi zinazoshiriki katika pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja".

New Zealand inafikiria kuongoza kujenga mradi wa safari za ndege na meli kutoka China hadi Latin Amerika kupitia China. Chini ya utaratibu wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja", wazo hilo limeifanya New Zealand kuwa kituo muhimu cha biashara na mawasiliano kati ya Asia na Latin Amerika. Kama mradi huo ukifaulu, utaleta fursa kubwa kwa nchi hiyo.

Waziri mkuu wa New Zealand Bibi Jacinda Ardern, amesema uhusiano kati ya China na New Zealand ni mzuri, katika sekta ya siasa, kuna uhusiano wa karibu; katika sekta ya uchumi, kuna ushirikiano katika mambo makubwa; na mawasiliano kati ya watu na watu yanaongezeka siku hadi siku. Pia amesema ingawa mazingira ya siasa ya kijiografia yemebadilika, sera ya kidiplomasia ya nchi hiyo itakuwa huru na kuwa na usawa.

Balozi wa China nchini New Zealand Bibi Wu Xi amesema, pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja" limetoa utaratibu kwa uhusiano wa ushirikiano kati ya nchi hizo mbili. Mwelekeo wa maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili umethibitisha tena, kushikilia wazo la kidiplomasia lenye uhuru na haki hakutakosa fursa ya ushirikiano wa kunufaishana.