Kujaribu kuibana China kwa suala la Taiwan hakika ni njia isiyopitika
2019-05-09 16:20:43| CRI

Baraza la Wawakilishi la Marekani Jumanne tarehe 7 lilipitisha "Sheria ya Uhakikisho ya Taiwan ya Mwaka 2019" na "Kurudia tena ahadi ya Marekani kwa Taiwan na kwa utekelezaji wa 'Sheria ya Uhusiano na Taiwan'". Hii ni mara nyingine kwa Marekani kuingilia ovyo masuala ya ndani ya China kwa kutumia suala la Taiwan, ambayo ni hatua ya kisiasa yenye hatari kubwa inayolenga kuzuia maendeleo ya amani ya China.

Hatua hiyo pia imeonyesha wazi kitendo kiovu cha baadhi ya wanasiasa wa Marekani wa kuchezea siasa. Kama Marekani itaendelea na mchezo huu, itaharibu vibaya sekta muhimu za ushirikiano kati ya China na Marekani, na pia itavuruga amani na utulivu katika Mlango Bahari wa Taiwan.

Wanasiasa wa Marekani wanatakiwa kufahamu kuwa kitendo chochote cha hatari cha kujaribu kuibana China kwa kutumia suala la Taiwan, hakika ni njia isiyopitika, kwani kitendo hicho ni makosa makubwa matatu.

Kosa la kwanza ni kuwa kitaharibu kabisa msingi wa maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizi mbili kubwa za China na Marekani, ambao umeelezwa wazi kwenye taarifa tatu za pamoja za China na Marekani wakati nchi hizo zilipoanzisha uhusiano wa kibalozi, yaani, duniani kuna China moja tu, China Bara na Taiwan zote ni sehemu ya China moja, na Jamhuri ya Watu wa China ni serikali pekee halali ya China.

Kosa la pili ni kuwa kinajaribu mstari wa mwisho wa China kwa kucheza "karata ya Taiwan". Suala la Taiwan linatumiwa na Marekani kila mara wakati uhusiano kati ya China na Marekani unapokumbwa na changamoto, ni kama karata ya mazungumzo, ya kutoa tishio au kuibana China. Lakini suala la Taiwan halipaswi kuchukuliwa kama karata ya kutatua mvutano wa China na Marekani, kwani suala la Taiwan ni suala la ndani la China, linahusu maslahi makuu ya taifa la China, uadilifu na hisia za wachina bilioni 1.4, na halitakiwi kuingiliwa na nchi yoyote, sembuse kutumiwa kwenye mvutano wa biashara.

Kosa la tatu ni kuwa kitendo hicho kitavuruga amani na utulivu wa Mlango Bahari wa Taiwan. Wanasiasa wa Marekani wanatakiwa kusoma kwa makini makala iliyoandikiwa na rais wa zamani wa Marekani Bw. Jimmy Carter mwaka huu kabla ya siku ya maadhimisho ya miaka 40 ya uhusiano wa kibalozi kati ya China na Marekani, na kutambua kuwa kama suala la Taiwan lisiposhughulikiwa ipasavyo, basi kuna uwezekano wa kuibuka kwa mgogoro wa kikanda, na kuleta madhara kwa dunia nzima.

Mwezi Aprili mwaka huu, rais wa sasa wa Marekani Donald Trump alimpigia simu Bw. Carter na kutaka kujua jinsi ya kuwasiliana na China. Habari zinasema moja ya mapendekezo yake ni "kutofanya vita". Lakini kama wanasiasa wanajaribu kuvuka mstari mwekundu wa China katika suala la Taiwan, ikiwemo kutuma manowari kisiwani Taiwan, hii itakuwa ni tarumbeta ya China ya kuirudisha Taiwan.