Marekani ni chanzo kikuu cha nakisi duniani
2019-05-20 20:02:05| CRI

"Kutoa shutuma zisizo na msingi" ni njia ya kawaida inayotumiwa na Marekani kushambulia washindani wake. Kwa mfano, kabla ya kufanyika kwa duru ya 11 ya mazungumzo ya uchumi na biashara kati ya China na Marekani, Marekani ilitoa shutuma zisizo na msingi kwamba China imerudi nyuma katika mazungumzo hayo, na kuzitumia kama kisingizio cha kuongeza ushuru dhidi ya bidhaa za China zinazouwa kwa Marekani.

Ili kuzuia maendeleo ya China na umwamba wa Marekani unaozidi kupungua, wanasiasa kadhaa wa Marekani wamesema uongo na kuilaumu China kufanya mashambulizi ya kiuchumi, kuiba teknolojia na kutaka kuwa mwamba duniani. Hoja mbalimbali za ajabu zisizo na msingi zimetenegeneza "tishio jipya la China", ambazo lengo lake ni kuficha ukweli kwamba Marekani ni chanzo kikuu cha nakisi duniani.

Wakati dunia ikikabiliwa na mabadiliko makubwa yasiyowahi kutokea katika miaka mia moja iliyopita, binadamu wanakaribisha duru mpya ya mapinduzi ya teknolojia, huku wakikabiliwa na misukosuko ya kifedha na kiuchumi. Jumuiya ya kimataifa inakabiliana na changamoto ya pamoja ya "Nakisi ya Usimamizi, Nakisi ya Uaminifu, Nakisi ya Amani, Nakisi ya Maendeleo." Marekani ikiwa nchi yenye nguvu kubwa zaidi duniani, haijafanya juhudi za kutosha kuondoa nakisi hizo, bali imekuwa chanzo kikuu cha nakisi hizo.

Kwa mfano, Marekani imeweka maslahi yake juu ya sheria na kanuni za pamoja za kimataifa na kutekeleza sera ya "Marekani Kwanza", huku ikijitoa kwenye makubaliano ya mfumo wa pande nyingi na kuongeza nakisi kwenye usimamizi wa dunia. Wakati huohuo, Marekani inajenga ukuta katika mpaka kati yake na Mexico, kuleta uchokozi Mashariki ya Kati, kubadilisha maoni katika ajenda kuu za dunia. Vitendo hivyo vimeleta wasiwasi juu ya kupamba moto kwa mikwaruzano ya kiuchumi na kibiashara duniani na mapambano ya siasa za kijiografia.

Mbali na hayo, Marekani inaonesha ubabe wake katika sehemu mbalimbali duniani. Nchi hiyo ilituma jeshi nchini Syria kwa kuukwepa Umoja wa Mataifa na kuichokoza Iran kupitia kutuma jeshi katika sehemu ya ghuba ya Persia. Marekani inaendelea kuleta maafa ya kibinadamu kote duniani na kuzidisha nakisi ya amani.

Ili kujilinda kibiashara na kiteknolojia, katika miaka ya hivi karibuni Marekani imetumia silaha ya ushuru kuwashambulia wenzi wakuu wa kibiashara, na kuweka vikwazo dhidi ya makampuni ya teknolojia za hali ya juu ikiwemo Huawei. Hatua hiyo imeharibu vibaya minyororo ya viwanda na thamani ya dunia, huku ikisababisha nakisi ya maendeleo duniani.

Kwa mujibu wa wazo la "Jumuiya ya kimataifa yenye mustakabali wa pamoja" lililotolewa na rais Xi Jinping wa China, shughuli za dunia zinatakiwa kusimamiwa na nchi mbalimbali duniani, kanuni za kimataifa zinatakiwa kuwekwa na nchi mbalimbali, na matunda ya maendeleo yanatakiwa kuzinufaisha nchi mbalimbali. Vitendo vya Marekani sio tu vinakwenda kinyume na mwelekeo wa kihistoria, mwelekeo wa dunia na maoni ya umma, bali pia vinaongeza nakisi za usimamizi wa ulimwengu.