Hatua ya Marekani ya kuongeza ushuru kwa bidhaa za China haishinikiza makampuni ya kimataifa nchini China
2019-05-23 17:04:14| CRI

Hivi karibuni Marekani imesema kutokana na hatua yake ya kuongeza ushuru kwa bidhaa za China, baadhi ya makampuni yatahamisha viwanda vyao kutoka China hadi Vietnam na nchi nyingine barani Asia, na baadhi ya makampuni ya Marekani yatarejea nchini humo. Kauli hizo zimekiuka kanuni za kawaida za uchumi za soko huria, na zimetungwa kwa makusudio na Marekani.

Hivi sasa uchumi wa China umebadilika na kupata maendeleo yenye ubora zaidi, na nafasi yake katika mnyonyoro wa viwanda na wa bei duniani umekuwa ukipanda hatua kwa hatua. Viwanda vya utengenezaji ambavyo viko kwenye kiwango cha kati na cha chini vimehamishia shughuli zake nchi za nje kuendana na kanuni ya maendeleo ya uhamishaji wa viwanda duniani, na si kutokana na hatua ya Marekani ya kuongeza ushuru kwa bidhaa za China kama Marekani ilivyodai. Lengo la kuchanganya mambo hayo mawili ni kuyashinikizia makampuni ya kimataifa kuondoka China na kuzuia ukuaji wa uchumi wa China.

Lakini takwimu halisi zimeonesha kuwa, Shirika la uendelezaji la biashara la Japan limetoa ripoti ikisema, katika mikakati ya makampuni ya Japan kuhusu uuzaji wa bidhaa nje, kwa upande wa uwekezaji na biashara ya kimataifa ya elektroniki, China inashika nafasi ya kwanza duniani. Waraka wa makampuni ya Marekani nchini China uliotolewa mwaka 2019 pia umeonesha kuwa, asilimia ya 98 ya makampuni ya Marekani yaliyohojiwa yanaeleza kuwa yataendelea kupanua soko la China.

Swali sasa ni kuwa, kwa nini hatua za Marekani ya kuongeza ushuru kwa bidhaa za China haziwezi kuyalazimisha makampuni ya Marekani kurudi nyumbani? Hii inatokana na kwamba, mitaji ya Marekani inawekezwa zaidi katika sekta ya utengenezaji yenye kiwango cha juu zikiwemo vifaa vya mawasiliano, kompyuta na vifaa vingine vya kielektroniki, ambazo zinahitaji wafanyakazi wengi wenye ustadi. China ikiwa nchi ya kipekee inayomiliki aina zote za viwanda duniani, si kama tu inaweza kutoa mnyororo kamili wa utoaji wa bidhaa na viwanda, bali pia ina kiasi kikubwa cha wafanyakazi wenye ustadi, hali ambayo imepunguza kwa kiasi kikubwa gharama za viwanda vya Marekani.

Mbali na hayo, China ina soko kubwa lenye idadi ya watu bilioni 1.4, na matumizi yamekuwa nguvu muhimu ya kuhimiza ongezeko la uchumi. La muhimu zaidi ni kwamba, na katika mwaka uliopita, China inaendelea kupanua ufunguaji mlango, hatua ambayo imeyatia imani kubwa kwa makampuni ya Marekani kuendelea na shughuli zao nchini China.

Kwa upande mwingine, Marekani imeongeza hali isiyo na utulivu na isiyotarajiwa kwenye soko kwa kupuuza maslahi ya watu na makampuni ya Marekani, kushikilia kuongeza ushuru kwa bidhaa za China. Tokea mwaka jana, makampuni ya Marekani yameanza kuhamisha mnyonyoro wa viwanda kutoka Marekani hadi nchi nyingine, ili kukidhi mahitaji ya soko la China na nchi nyingine duniani.

Kutokana na hayo, hatua ya Marekani ya kuongeza ushuru kwa bidhaa za China haiwezi kushinikizia makampuni ya kimataifa nchini China kuondoka kutoka China, bali itayalazimisha makampuni ya Marekani yaondoke nchini Marekani kwenda nchi nyingine duniani, na kuongeza mgogoro wa viwanda nchini Marekani, na chanzo kikuu ni watunga sea wa Marekani wanaoshikilia kithabiti "wazo wenye msimamo kali la kujitafutia faida".