Jaribio la kuzuia soko kubwa lenye idadi ya watu bilioni 1.4 kamwe halitafanikiwa
2019-05-24 19:54:49| CRI

Hivi karibuni makampuni mengi yametangaza kwa kauli kwamba yamesimamisha ushirikiano na Kampuni ya Huawei ni uvumi, hali ambayo imeonesha kuwa hatua ya Marekani ya kudhibiti uuzaji wa bidhaa wa Kampuni ya Huawei, imeharibu maslahi ya makampuni mengi ya nchi za nje yakiwemo yale ya Marekani, na haiungwi mkono na wananchi wake. Jaribio la baadhi ya wanasiasa wa Marekani la kuwekea vizuizi dhidi ya soko kubwa la China lenye idadi ya watu bilioni 1.4 halitafanikiwa.

Sababu ya Makampuni hayo yakiwemo kampuni ya Panasonic, Hitachi za Japan, Kampuni ya Infineon ya Ujerumani, na Kampuni ya mawasiliano ya simu ya Uingereza EE ya kuthibitisha kwamba hayasimamishi ushirikiano na Kampuni ya Huawei inatokana na kwamba, vitendo wa kimwamba vilivyochukuliwa na Marekani havina msingi na vimekiuka kanuni za uchumi wa soko huria, na kudhuru vibaya maslahi zao zenyewe.

Marekani inachukua hatua mbili kwa wakati mmoja: inaongeza ushuru kwa bidhaa za China zinazouzwa nchini Marekani, huku ikisambaza uvumi. Hata hivyo thamani ya biashara ya China na nchi za nje inaongezeka. Katika miezi minne iliyopita, matumizi halisi ya mitaji ya kigeni ya China yameongezeka kwa asilimia 6.4, thamani ya jumla ya uagizaji na uuzaji wa bidhaa nje imeongezeka kwa asilimia 4.3 kuliko mwaka jana wakati kama huu. Wakati huo huo ongezeko la thamani ya biashara ya nchi zinazojiunga na ujenzi wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja" wa China limefikia asilimia 9.1, kiasi ambacho kimezidi kwa asilimia 4.8 kuliko kiwango cha jumla cha biashara ya nje. Mbali na hayo, China imesaini makubaliano ya ushirikiano yenye thamani zaidi ya dola za kimarekani bilioni 64 kwenye Mkutano wa pili wa Baraza la ushirikiano wa kimataifa la "Ukanda Mmoja, Njia Moja". Hali ambayo imeongeza uwezo wa China wa kukabiliana na tishio la kiuchumi. Mnyororo wa viwanda duniani unaoundwa kutokana na matakwa ya kujiendeleza ya nchi mbalimbali na kanuni ya uchumi wa soko hautakatizwa na Marekani.

Licha ya hayo, kuanzia mwaka 2008 hadi 2017, mahitaji ya ndani ya China yamechangia kwa zaidi ya asilimia 100 kwa ongezeko la uchumi la China kwa mwaka, na kuwa nguzo muhimu ya kuhimiza maendeleo ya uchumi. Kwa upande mwingine, kiwango cha utegemezi wa biashara ya nje cha China kimepungua hadi asilimia 33. Hali ambayo imeonesha kuwa kutokana na mahitaji makubwa ya ndani, na mageuzi ya kimuundo katika upande wa utoaji wa bidhaa, China inaunda soko lenye nguvu kubwa zaidi la ndani, na kuhimiza viwanda na uwezo wa ushindani wa makampuni hadi kwenye kiwango cha juu zaidi.

Hadi sasa mafungamano ya kiuchumi yanapozidi kupata maendeleo, uchumi wa dunia hautarudi nyuma, na uchumi wa China una uwezo wa kukabiliana na changamoto mbalimbali. Bila ya kujali jinsi Marekani inavyoweka shinikizo, China inayosukuma mbele mageuzi na ufunguaji mlango kwa hatua thabiti, itafunga mlango wazi kwa dunia, na kuwa soko linalovutia kwa wingi uwekezaji na biashara ya dunia. Wakati huo huo, wanasiasa wa Marekani wanaharakisha mchakato wa kuelekea kuwa kisiwa kilichojitenga na dunia.