Rais Xi Jinping wa China leo ameondoka kwenda Russia kwa ziara rasmi nchini humo na kuhudhuria mkutano wa 23 wa Baraza la Uchumi Duniani la St. Petersburg. Huu ni mwaka wa 70 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati ya China na Russia, pande hizo mbili zimeeleza mara nyingi kuwa, uhusiano kati yao uko katika kipindi kizuri zaidi kwenye historia. Ziara ya rais Xi inayofanyika katika wakati huo muhimu itahimiza uhusiano kati ya pande hizo mbili kwenye kiwango cha juu zaidi na kupata maendeleo makubwa zaidi.
Viongozi wa China na Russia wamekutana kwa mara zaidi ya 20 katika miaka mitano iliyopita, na kuanzisha uhusiano wa karibu wa kikazi na urafiki mwema wa binafsi. Wakati hali ya kimataifa inapokabiliwa na mabadiliko yenye utatanishi mkubwa, pande hizo mbili siku zote zinaheshimiana, kutoingiliana mambo ya ndani, na kuungana mkono katika maslahi kuu na masuala zinazoyafuatilia kwa pamoja. Hii ni sababu muhimu kwa uhusiano kati ya China na Russia kupata maendeleo kwa hatua madhubuti, na uhusiano kati ya pande hizo mbili vilevile umekuwa uhusiano wenye kiwango cha juu zaidi cha kuaminiana, kushirikiana na pia kuwa na thamani kubwa zaidi ya kimkakati.
Wakati Maadhimisho ya miaka 70 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati ya pande hizo mbili yanapokaribia, ushirikiano kati ya nchi hizo mbili utapata maendeleo mapya. Katika wiki iliyopita, daraja la kwanza la barabara kati ya mipaka ya nchi hizo mbili limejengwa, ujenzi wa daraja la kwanza la reli pia utakamilika, na mabomba ya kusafirisha gesi asilia kati ya nchi hizo mbili yataanza kufanya kazi ndani ya mwaka huu. Ushirikiano kati ya pande hizo mbili umehusisha sekta mbalimbali zikiwemo nishati, ujenzi wa miundo mbinu, sayansi na teknolojia za hali ya juu, biashara ya kieleketroniki, kilimo, uendelezaji wa eneo la Aktiki na ushirikiano wa kikanda. Msemaji wa rais wa Russia Bw. Dmitry Peskov pia ameeleza kuwa uwekezaji wa China nchini Russia utakuwa na ongezeko kubwa.