Mazingira yenye usalama na urafiki ni njia pekee inayowavutia watalii wa China
2019-06-04 20:44:24| CRI

Wizara ya mambo ya nje ya China leo imetoa tahadhari ya usalama kuhusu kwenda nchini Marekani ikisema, kutokana na idara za sheria za Marekani kuwasumbua mara nyingi raia wa China kupitia ukaguzi wa kuingia na kutoka nchini humo na mahojiano, hivyo wizara hiyo inawakumbusha raia wa China wanaoenda Marekani na matawi ya mashirika ya China nchini Marekani kuinua kiwango cha wazo la usalama. Wizara ya utamaduni na utalii ya China pia imetoa tahadhari ya kwenda kutalii nchini Marekani ikisema, kutokana na ongezeko la matukio ya ufyatuliaji wa risasi, uporaji na wizi nchini Marekani, wizara hiyo inawakumbusha watalii wa China kutathmini hatari ya kutalii nchini Marekani.

Muda wa tahadhari hizo mbili utadumu mpaka mwishoni mwa mwaka huu. Tahadhari hizo zimeonesha kuwa Marekani ikiwa chaguo kuu la raia wa China kutalii katika nchi za nje, hali ya usalama inazidi kuwa mbaya, hatari ya utalii inaongezeka, hata upendeleo na ubaguzi wa utekelezaji wa sheria pia unaongezeka. Hali hiyo sio tu inatishia usalama wa raia wa China, bali pia inadhuru maslahi halali ya raia wa China, hivyo idara husika za China hazina budi kutoa tahadhari za usalama.

Kufuatia China kuzidi kufungua mlango na kiwango cha matumizi kuendelea kuongezeka, idadi ya wachina wanaofanya kazi na kutalii katika nchi za nje inaongezeka siku hadi siku. Mwaka jana idadi ya raia wa China waliotalii nchi za nje ilifikia milioni 150, ambayo inaongezeka kwa asilimia 14.7 ikilinganishwa na mwaka jana. China inaendelea kushika nafasi ya kwanza katika nchi zenye raia wengi zaidi wanaotalii nchi za nje duniani. Lakini idadi ya wachina wanaotalii nchini Marekani ilipungua kwa asilimia 5.7 ambayo ilipungua kwa mara ya kwanza katika miaka 15 iliyopita. Chanzo cha hali hiyo ni hali ya usalama ya Marekani inayoendelea kuwa mbaya.

Wakati huohuo, upendeleo na ubaguzi wa utekelezaji wa sheria wa Marekani pia unaongezeka kwa udhahiri. Hivi karibuni raia wengi wa China walisumbuliwa na kukaguliwa bila ya sababu na idara za sheria za Marekani wakati wakiingia au wakiwa nchini humo. Mbali na hayo, wanasiasa kadhaa wa Marekani wanamchukulia kila mchina kama jasusi, na kutaka kuwafanya wananchi wa Marekani kuwaogopa wachina.

Kwa mujibu wa makadirio ya Marekani, idadi ya watalii wa China watakaoenda nchini Marekani itafikia milioni 3.3 mwaka huu, na kuongezeka hadi milioni 4.1 ifikapo mwaka 2023. Lakini kufuatia hali ya hivi sasa, lengo hilo halitaweza kutimizwa. Ili kuwavutia watalii wa China, wadau wa Marekani wamefanya juhudi kubwa, ikiwemo kuwaajiri wafanyakazi wanaojua kichina, kutoa chakula cha kichina na kutoa vijitabu vya kichina kuhusu utalii wa Marekani. Lakini hatua hizo haziwezi kuondoa athari mbaya zinazoletwa na sera zenye msimamo mkali zinazochukuliwa na wanasiasa wa Marekani.