Uhusiano kati ya China na Russia waingia katika zama mpya
2019-06-07 16:40:49| CRI

Rais Xi Jinping wa China ambaye yupo Moscow, amesaini taarifa mbili muhimu za pamoja na rais Vladimir Putin wa Russia, wakitangaza kukuza uhusiano wa kiwenzi na ushirikiano wa kimkakati wa pande zote kati ya pande hizo mbili katika zama mpya, na kushirikiana katika kuimarisha utulivu wa kimkakati duniani.

Huu ni mwaka wa 70 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati ya China na Russia. Uhusiano kati ya nchi hizo mbili umeendelezwa na kuwa mfano mzuri wa kuigwa wa uhusiano wa kijirani na ule wa nchi kubwa kwa kuwa na kiwango cha juu zaidi cha kuaminiana, kushirikiana na wenye thamani ya juu zaidi ya kimkakati. Viongozi wa nchi hizo mbili wamesisitiza mara nyingi kubwa, hivi sasa uhusiano kati ya nchi hizo mbili uko katika kiwango cha juu zaidi katika historia.

Kutokana na kukabiliwa na mabadiliko makubwa ambayo hayajawahi kutokea katika miaka mia moja iliyopita duniani, uhusiano kati ya China na Russia umepanda ngazi na kuwa "uhusiano wa kiwenzi na ushirikiano wa kimkakati wa pande zote katika zama mpya", ukionesha kuwa uhusiano kati ya nchi hizo mbili umeinuka katika kiwango cha juu cha kimkakati ambacho hakijawahi kufikia hapo zamani, na utakuwa na athari kubwa kwa ushirikiano kati ya pande mbili na utaratibu wa dunia.

Uhusiano kati ya nchi hizo mbili kuingia katika zama utawanufaisha zaidi watu wa nchi hizo mbili. Mwaka jana thamani ya biashara kati ya China na Russia ilizidi dola za kimarekani bilioni 100, ikiwa ni ongezeko la zaidi ya asilimia 27 kuliko mwaka 2017 wakati kama huu. Kukabiliana na kupungua kwa ongezeko la uwekezaji wa biashara, huku vitendo vya kujilinda kibiashara vikizidi kuongezeka, si rahisi kupata matokeo hayo.

Uhusiano kati ya pande hizo mbili kuingia katika zama mpya, pia kunamaanisha kuwa nchi hizo mbili zitaimarisha uratibu na ushirikiano katika mambo ya kimataifa, kutoa mapendekezo mengi zaidi ya China na Russia, na kulinda vizuri zaidi kanuni za utaratibu wa pande nyingi.

China na Russia zikiwa nchi wajumbe wa kudumu kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, zina msimamo sawasawa au unaofanana katika masuala muhimu duniani. Katika miaka 6 iliyopita, viongozi wa nchi hizo mbili wamefanya mazungumzo kwa mara zaidi ya 20, wakifanya uratibu na majadiliano yenye ufanisi kuhusu masuala muhimu ya kimataifa.

Uhusiano wa kimkakati kati ya China na Russia unaofuata msingi wa kuaminiana kisiasa umekuwa mfano mzuri wa kuigwa kwa uhusiano kati ya nchi kubwa duniani. Uhusiano huo utafikia kiwango cha juu zaidi na kupata maendeleo makubwa zaidi, kuwaletea wananchi wa nchi hizo mbili faida kubwa zaidi, na kuchangia utulivu katika utaratibu wa kimataifa ambao unakabiliwa na mabadiliko yenye utatanishi.