Kujenga jumuiya yenye mustakabali mzuri ya SCO iliyo na uhusiano wa karibu zaidi
2019-06-15 20:11:57| CRI

Rais Xi Jinping wa China ametoa hotuba kwenye Mkutano wa 19 wa Baraza la viongozi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai SCO uliofanyika jana, akitoa wito wa kuijenga jumuiya hiyo iwe jumuiya yenye mustakabali wa pamoja ambayo wanachama wake wanashirikiana na kuaminiana, kukabiliana na changamoto kwa pamoja, kusaidiana na kunufaishana, kusikilizana na kufundishana, na kuwa na uhusiano wa karibu zaidi. Hayo ni mapendekezo yaliyotolewa na rais Xi Jinping wa China kuhusu maendeleo ya jumuiya hiyo baada ya mkutano wa viongozi wa jumuiya hiyo iliyofanyika mwaka jana mjini Qingdao, hatua ambayo imeonesha uungaji mkono wa China kwa jumuiya hiyo.

Kutokana na maendeleo ya miaka 18, Jumuiya ya SCO imekuwa shirika la kimataifa la kikanda linalohusisha idadi kubwa zaidi na maeneo makubwa zaidi duniani, na kuwa nguvu muhimu ya kuhimiza amani na maendeleo ya dunia, na kulinda usawa na haki ya kimataifa. Hivi sasa hali ya dunia inaonesha utatanishi mkubwa, jinsi gani kwa jumuiya hiyo inavyotumia fursa nzuri na kukabiliana na changamoto mbalimbali, ni suala muhimu katika kuingia mwanzo mpya wa maendeleo.

Mapendekezo aliyotoa rais Xi kwenye mkutano huo yana mambo mapya kutokana na mabadiliko ya hali ya kimataifa na kikanda.

Pendekezo lake kuhusu kuijenga jumuiya ya SCO kuwa mfano wa kuigwa wa kushirikiana na kuaminiana lina umuhimu katika kukabiliana na migogoro ya ushindani wa kimataifa na wa kisiasa inapoongezeka. Uaminifu ni njia nzuri ya kuunganisha uhusiano wa kimataifa, kushirikiana na kuaminiana kwa nchi wanachama wa jumuiya ya SCO, kutasaidia kupunguza nakisi ya uaminifu duniani.

Pendekezo la rais Xi kuhusu kukabiliana kwa pamoja changamoto mbalimbali linaweka mkazo katika kujenga mazingira yenye usalama na utulivu. Rais Xi amesisitiza kushikilia wazo la kupata maendeleo kwa pamoja, kushirikiana na la kudumu, kuzuia kwa ufanisi mwelekeo wa mawazo yenye siasa kali.

Pendekezo kuhusu kuijenga jumuiya ya SCO kuwa kusaidiana na kunufaishana, kumeonesha matakwa ya nchi wanachama wa jumuiya hiyo ya kujiendeleza. Rais Xi amesisitiza kulinda utaratibu wa biashara ya pande nyingi, kujenga kwa pamoja uchumi wa dunia ulio wazi, na kuhimiza uoanishaji kati ya pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" na mikakati ya maendeleo ya nchi mbalimbali na mipango ya ushirikiano wa kikanda.

Pendekezo kuhusu kuijenga jumuiya ya SCO kuwa ya kusikilizana na kufundishana, linalenga kuingiza injini ya kudumu kwenye maendeleo ya jumuiya hiyo. Rais Xi ametoa mapendekezo ya kuimarisha ushirikiano katika sekta za utamaduni, elimu, utalii, michezo na vyombo vya habari.

Jumuiya ya SCO kujihusisha katika kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja iliyo na uhusiano wa karibu zaidi, kutakuwa na umuhimu mkubwa katika kukabiliana na changamoto zinazoongezeka siku hadi siku duniani, na kulinda utaratibu wa pande nyingi na kanuni za kimataifa.