Kuivuruga Hongkong hakutaleta faida yoyote kwa pande zote
2019-06-15 17:32:39| CRI

Hivi karibuni baadhi ya wabunge wa Marekani walitaja "Sheria kuhusu haki za binadamu na demokrasia ya Hong kong" ambayo iliwekwa kando, wakiitaka serikali ya Marekani ithibitishe hali ya kujitawala kwa Hong Kong kila mwaka, ili kuamua kama itaendelea kuipa Hong Kong haki maalumu ikiwa eneo huru la ushuru wa forodha kwa kufuata Sheria ya Sera ya Marekani-Hongkong ya mwaka 1992. Kuingilia kwa nguvu kwa baadhi ya wanasiasa mambo ya ndani ya China, kumeonesha vya kutosha jaribio la Marekani la kuzuia maendeleo ya China na kuiwekea vikwazo kwa pande zote. Lakini watu wenye busara wanatambua kwamba, vitendo hivyo havitaleta faida yoyote kwa pande zote.

Kwa kweli Sheria ya sera ya Marekani-Hongkong ni njia ya Marekani ya kuingilia kati mambo ya ndani ya China. Kila mwaka Marekani inatangaza ripoti ya kuhusu mambo mbalimbali ya Hongkong kabla ya kurudi China na baada ya kurudi China. Kutokana na kupamba moto kwa migogoro ya kibiashara kati ya China na Marekani, baraza la juu la bunge la Marekani limepitisha sheria kuhusu haki za binadamu na demokrasia ya Hongkong, lengo lake ni kuendelea kuweka shinikizo dhidi ya China kwa kisingizio cha kutathmini kama Hongkong inapewa manufaa maalumu.

Vitendo vya kuivuruga Hongkong, havitaleta faida yoyote kwa pande zote ikiwemo Marekani. Marekani ikiwa moja ya wenzi muhimu wa biashara wa Hongkong, ustawi na utulivu wake unalingana na maslahi ya Marekani. Tangu mwaka 2009, Marekani imepata urari mzuri na biashara wenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 297 kupitia biashara kati yake na Hongkong, ambao ni urari mzuri wenye thamani kubwa zaidi duniani. Hongkong ni sehemu inayovutia uwekezaji wa moja kwa moja kutoka Marekani. Endapo ustawi na utulivu wa Hongkong utaharibiwa, maslahi ya makampuni ya Hongkong na Marekani yataathiriwa vibaya.

Mambo ya Hongkong ni mambo ya ndani ya China ambayo hayapaswi kuingiliwa na nchi nyingine yoyote na makundi ya nje. China kamwe haitavumilia nguvu za nje kuingilia ndani mambo ya Hongkong na ya China. Wanasiasa wa Marekani wanatakiwa kutambua wazi kwamba, kuivuruga Hongkong hakutaleta faida kwa pande zote, na kwamba wanatakiwa kufanya mambo ya kusaidia kuaminiana na kushirikiana kati ya China na Marekani.