Rais Xi Jinping wa China atoa wito wa kujenga mustakabali mzuri wa Asia na dunia nzima
2019-06-16 16:41:43| CRI

Rais Xi Jinping wa China ametoa hotuba muhimu kwenye Mkutano wa tano wa viongozi kuhusu ushirikiano na kujenga uaminifu barani Asia CICA huko Dushanbe, Tajikistan, akitoa mapendekezo na msimamo wa China kuhusu jinsi nchi za Asia zitakavyokabiliana na changamoto za pamoja, kujenga Jumuiya ya Asia yenye mustakabali wa pamoja, na kupata mustakabali mzuri katika siku za baadaye.

Bara la Asia lina theluthi moja ya ardhi na theluthi mbili ya idadi ya watu duniani, makabila zaidi ya 1000 na theluthi moja ya thamani ya jumla ya uchumi duniani. Ikiwa moja ya sehemu zenye uhai na mustakabali mkubwa zaidi duniani, bara la Asia vilevile linakabiliana na changamoto za pamoja zikiwemo ukosefu wa kuaminiana kisiasa, kutokuwepo kwa uwiano wa maendeleo ya uchumi, na masuala ya usalama na utawala. Mkutano wa CICA ulioanzishwa miaka 27 iliyopita unalenga kuongeza kuaminiana na kushirikiana kati ya nchi mbalimbali, na kulinda amani na utulivu kwenye kanda hiyo.

Kwenye hotuba aliyotoa rais Xi, ameeleza matarajio yake kwa bara la Asia, na kutoa pendekezo la kujenga Asia inayoheshimiana na kuaminiana, yenye usalama na utulivu, maendeleo na ustawi, iliyo wazi na shirikishi, na kufanya uvumbuzi kwa ushirikiano, hali ambayo inahitaji juhudi za pamoja za pande zote, ili kutatua masuala ya kuaminiana, amani, maendeleo na utawala.

Ingawa China haitashika uenyekiti wa Mkutano wa CICA, lakini ikiwa moja kati ya familia ya bara la Asia na nchi kubwa inayowajibika, China siku zote ni mjenzi wa amani ya dunia, mchangiaji wa maendeleo ya dunia na mlinzi wa utaratibu wa kimataifa, na kutekeleza jukumu la kuhimiza kujenga uhusiano wa aina mpya wa kimataifa, na jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.

Katika hotuba aliyoitoa kwenye Mkutano wa viongozi wa CICA uliofanyika mjini Dushanbe, rais Xi amesisitiza tena nia na hatua za China kushikilia njia ya kujiendeleza kwa amani, na kwamba China itafuata wazo la usimamizi wa mambo ya dunia kwa msingi wa kujadiliana, kujenga na kunufaika kwa pamoja, kulinda kithabiti utaratibu wa kimataifa ambao kiini chake ni Umoja wa Mataifa, na utaratibu wa biashara wa pande nyingi ambao kiini chake ni Shirika la biashara duniani WTO, kupinga kithabiti kujilinda kibiashara, utaratibu wa upande mmoja, ili kulinda haki halali ya maendeleo ya nchi mbalimbali, na usawa na haki za kimataifa.

Mkutano wa CICA ukiwa baraza la pande nyingi linalohusiana na usalama, madhumuni yake ni kuamua hatua za kuimarisha kuaminiana kati ya pande nyingi, kuongeza mazungumzo na ushirikiano, na kuhimiza amani, usalama na utulivu barani Asia. Hotuba aliyoitoa rais Xi Jinping pamoja na michango ya China kwa ajili ya mkutano wa CICA katika miaka mingi iliyopita, itasaidia kutia moyo kwa pande mbalimbali mkutano huo kufanya juhudi katika kutafuta amani, utulivu na ustawi, kuimarisha msingi wa mazungumzo na ushirikiano, kukabiliana na changamoto kwa hatua za pamoja, ili kujenga mustakabali mzuri wa Asia na dunia nzima.