Soko la hisa la China lapiga hatua muhimu katika kufungua mlango na nchi za nje
2019-06-17 19:00:30| CRI

Utaratibu wa kuunganisha soko la hisa ya Shanghai na la London, umeanzishwa rasmi leo mjini London, ikiwa ni baada ya maandalizi ya miaka minne. Hii ni hatua muhimu kwa soko la hisa la China kutimiza kufungua mlango kwa nchi za nje, hatua ambayo itachangia maendeleo ya masoko ya hisa ya nchi zote mbili za China na Uingereza, na utaratibu huo wa kivumbuzi umeonesha nia na vitendo halisi kwa soko la hisa la China kupanua ufunguaji mlango kwa dunia.

Utaratibu wa kuunganisha soko la hisa la Shanghai na la London uliotolewa kwenye Mazungumzo ya 7 ya uchumi na fedha kati ya China na Uingereza yaliyofanyika mwezi Septemba mwaka 2015, kiini chake ni kupanua kufungua mlango kwa soko la hisa la China na nchi za nje. Kutokana na utaratibu huo, makampuni yanayoorodheshwa kwenye soko la hisa ya sehemu hizo mbili, yataweza kutoa cheti cha DR na kufanya biashara katika soko la hisa la upande mwingine.

Kuanzishwa kwa utaratibu huo kutasaidia kulinganisha mfumo wa soko la hisa la China na soko la kimataifa, na kuongeza uwezo wake wa ushindani, vilevile una umuhimu mkubwa kwa wawekezaji wa kimataifa na soko la hisa la Uingereza. Hivi sasa kuna idadi kubwa ya makampuni ya China yanayoorodheshwa kwenye soko la hisa, kutokana na utaratibu huo, wawekezaji wa nchi za nje watakuwa na fursa za kuwekeza moja kwa moja kwenye makampuni hayo ya China yenye sifa bora, na kufaidika kutokana na ukuaji wa makampuni hayo. Mbali na hayo, kutokana na kuwa Uingereza iko kwenye mchakato wa kujitoa kutoka Umoja wa Ulaya, uzinduzi wa utaratibu huo una umuhimu kwa soko la hisa la London kuimarisha hadhi yake, ikiwa ni taasisi kubwa zaidi ya hisa barani Ulaya, na kituo cha fedha duniani.

Mazungumzo ya kumi ya uchumi na fedha kati ya China na Uingereza pia yamefanyika hii leo mjini London. Pande hizo mbili zimefanya majadiliano kuhusu hali ya jumla ya uchumi, usimamizi wa uchumi duniani, uwekezaji wa biashara na ushirikiano wa miradi mikubwa, ushirikiano wa fedha pamoja na ushirikiano wa kimkakati na katika sekta mpya. Inakadiriwa kuwa, uzinduzi wa utaratibu wa kuyaunganisha masoko ya hisa ya Shanghai na London, utazidi kuimarisha ushirikiano wa fedha kati ya China na Uingereza, na kujenga kwa pamoja zama yenye mustakabali mzuri kati ya pande hizo mbili.