Hakuna vikwazo vitakavyozuia hatua ya China ya kufanya uvumbuzi wa sayansi na teknolojia
2019-06-18 16:47:01| CRI

Hivi karibuni mshindi wa Tuzo ya Nobel Bibi Tu Youyou na kikundi chake wametangaza matokeo mapya ya utafiti, na kutoa mpango wa kutatua tatizo la usugu wa vimelea vya malaria dhidi ya dawa ya artemisinin. Huu ni mchango mpya unaotolewa na wanasayansi wa China katika kutatua matatizo ya matibabu ya binadamu. Maelfu ya wanasayansi wa China wanaojihusisha kwa bidii katika utafiti wa sayansi na teknolojia ni siri ya China ya kupata maendeleo katika sekta hiyo.

Lakini baadhi ya wamarekani wana wasiwasi juu ya uvumbuzi huo wa sayansi na teknolojia wa China. Badala ya kufikiria namna ya kuongeza uwezo wake wa ushindani katika sekta hiyo, wanapendelea kusambaza uvumi, na kuipaka matope China. Mwishoni mwa mwezi April mwaka huu, mkurugenzi wa Idara ya upelelezi ya jinai ya Marekani FBI Bw. Christopher Wray alidai kwamba, China "iliihamasisha raia wake kuiba hakimiliki za ubunifu za Marekani, kwa kupitia makampuni, vyuo vikuu na mashirika mbalimbali." Hivi karibuni imewazuia wanafunzi wanaotaka kwenda kusoma Marekani, na kuweka vikwazo kwa makampuni ya China kuingia katika soko la nchi hiyo na makampuni ya China ikiwemo Huawei, kwa kisingizio cha "Usalama wa nchi", ili kuiwezesha Marekani idumishe hadhi yake ya kutawala katika sekta ya teknolojia na mnyororo wa viwanda.

Lakini hatua ya China ya kufanya uvumbuzi wa sayansi na teknolojia haitaweza kuzuiliwa. Katika miaka 40 iliyopita tangu sera ya mageuzi na ufunguaji mlango ianze kutekelezwa, maelfu ya wanasayansi wa China wamefanya juhudi za kujiendeleza kwa kujitegemea, na kutoa mchango muhimu katika kukabiliana na matatizo mbalimbali duniani.

Kwa mfano, dawa ya malaria iitwayo artemisinin iliyogunduliwa na China imewasaidia mamilioni ya wagonjwa wa malaria barani Afrika, mchele wa kisasa umetatua tatizo la chakula kwa dunia yenye idadi ya watu milioni kadhaa, urushaji wa satelaiti ya majaribio ya kisayansi "Mozi" umechangia katika kujenga mtandao wa usalama na upashanaji wa habari duniani, na urushaji wa satelaiti ya "Chang'e No. 4" kwenye sayari ya mwezi umesaidia binadamu kufahamu vizuri zaidi sayari hiyo. Katika Mkutano wa Baraza la uchumi la kimataifa la St. Petersburg uliofanyika hivi karibuni, rais Xi Jinping wa China ameeleza kuwa China ingependa kubadilishana matokeo mapya ya sayansi na teknolojia ikiwemo 5G, hatua ambayo itasaidia dunia nzima kuandaa kwa pamoja uwezo mkubwa wa ushindani, na kubadilisha njia ya kupata ukuaji wa uchumi.

China siku zote inachukua msimamo wa wazi na shirikishi kwa ushirikiano wa sayansi na teknolojia duniani. Sasa itatumia njia gani kukabiliana na vitisho vya Marekani? Hivi sasa baadhi ya waMarekani wamesahau jinsi nchi yao ilivyojiendeleza na kuwa na nguvu, na kuzuia maendeleo ya sayansi na teknolojia ya nchi nyingine. Hatua yake hii itaweza tu kuongeza nia kwa nchi mbalimbali ikiwemo China kufanya uvumbuzi, na kuunganishwa kuwa msukumo mkubwa zaidi wa kuhimiza maendeleo ya sayansi na teknolojia.