Mali za China zimekuwa sehemu muhimu za mitaji ya kimataifa
2019-06-21 20:48:09| CRI

Baada ya soko la hisa la China kufungwa leo, kampuni ya kutunga vigezo ya pili kwa ukubwa duniani FTSE Russell imeweka Hisa A ambayo ni hisa ya RMB katika mfululizo wa vigezo vya hisa kote duniani. Hii ni habari nyingine njema kwa soko la mitaji la China baada ya kampuni kubwa zaidi ya kutunga vigezo duniani MSCI kuinua kiwango cha Hisa A. Hii inamaanisha kuwa wawekezaji wa kimataifa sio tu wanaendelea kudumisha mahitaji ya uwekezaji kwa soko la mitaji la China, bali pia wana imani na mustakabali wa uchumi wa China.

China ikiwa nchi ya pili kwa ukubwa wa uchumi duniani, soko lake la mitaji siku zote ni sehemu isiyoweza kukosekana katika sehemu za mitaji ya kimataifa. Hivi sasa kutokana na athari zinazoletwa na mikwaruzano ya kibiashara, hali isiyo hakika ya soko la kimataifa inaongezeka. Katika mustakabali huo, uchumi wa China bado unaendelea kwa utulivu, hatari ya soko la mitaji la China iko katika kiwango cha chini. Hivyo soko la mitaji la China limewavutia wawekezaji wengi wa kimataifa, ambao wanalichukulia soko hilo kama bandari salama. Hii pia ni sababu muhimu kwa kampuni mbili kubwa zaidi za kutunga vigezo duniani kutilia maanani katika Hisa A.

Nyuma ya kampuni hizo mbili, kuna wawekezaji wanaosimamia mali za dola bilioni 2500 za kimarekani kote duniani. Hatua hizo zitawawezesha wawekezaji hao kununua mali za Hisa A kwa ufanisi. Hivi sasa, katika soko la hisa na dhamana la China, kiwango cha mitaji ya kigeni ni asilimia 2 hadi 3 hivi, hivyo inamaanisha mitaji ya kigeni ina nafasi kubwa ya kuingia katika soko la mitaji la China.

Kuingia kwa mitaji ya kimataifa katika soko la Hisa A la China ni kura ya imani iliyopigwa kwa China kuzidi kufungua mlango na kushirikiana kwa kina na soko la fedha la kimataifa. Aidha, hii imethibitisha kuwa wawekezaji wa kimataifa wana matarajio mazuri na mustakabali wa maendeleo ya kiuchumi ya China.