China yatangaza Hatua mpya za usimamizi kuhusu masharti ya uwekezaji kwa kampuni kutoka nje
2019-07-01 17:35:39| CRI

Serikali ya China jana ilitangaza rasmi Hatua maalumu za usimamizi kuhusu masharti ya uwekezaji kwa kampuni za kigeni, pamoja na Hatua maalumu za usimamizi kuhusu masharti ya uwekezaji wa kampuni hizo kwenye Eneo la Biashara Huria, ikiwaruhusu wafanyabiashara kutoka nje kuwekeza kwa upande wake pekee katika sekta nyingi zaidi nchini China.

Katika miaka ya hivi karibuni,China imefanya mageuzi kwa kina na kwa pande zote, kufungua mlango zaidi, na kuchukua hatua za kupunguza masharti kwa uwekezaji wa kampuni za nje, na itaondoa kwa pande zote vizuizi vingine vilivyowekwa kwenye Hatua za usimamizi kuhusu masharti ya uwekezaji kwa kampuni kutoka nje.

Mbali na hayo, ufunguaji mlango vilevile ni chaguo la lazima kwa China katika kutafuta maendeleo ya uchumi yenye sifa bora na kuwanufaisha zaidi wananchi. Katika miaka ya hivi karibuni, viwanda vya utengenezaji vya China vimefungua mlango kwa uwekezaji wa kigeni, hatua ambayo imeharakishwa katika sekta ya utoaji wa huduma, na itasaidia kuinua kiwango cha maendeleo ya viwanda vinavyohusika vya China, na kuzihimiza kampuni za nchi hiyo kupata uwezo mkubwa katika ushindani, na kuwanufaisha wananchi zaidi.

Toleo jipya la Hatua maalumu za usimamizi kuhusu masharti ya uwekezaji kwa kampuni kutoka nje litatoa maendeleo mapya kwa uwekezaji wa nchi nje nchini China. Hivi sasa, kampuni za nje zimeiletea China zaidi ya nusu ya thamani ya biashara na nje.

Tokea mwaka huu, migogoro ya biashara inayozidi kuongezeka imeleta changamoto kubwa kwa mnyororo wa viwanda, thamani na utoaji wa bidhaa duniani. China ikiwa nchi kubwa ya biashara ya mizigo duniani, nchi ya pili kwa uchumi duniani, inafuatiliwa sana na watu kuweza kujua itachukua hatua gani kuwa nguzo ya kutuliza mazingira yasiyoweza kutarajiwa. Waraka kuhusu uchumi wa China na kampuni za Japan wa mwaka 2019 umeeleza kuwa, kampuni za Japan nchini China zinatarajia soko la China lifungue mlango zaidi.

Toleo hilo jipya si kama tu limeonesha hatua halisi za China katika kufungua mlango zaidi, pia limetoa thibitisho la kisera kwa uwekezaji wa nchi za nje kuingia nchini China, kunufaika kwa pamoja na fursa za maendeleo za China.

Ukweli umethibitisha kwa mara nyingine kuwa, bila ya kujali dunia itapata mabadiliko gani, uchumi wa China utadumisha utulivu na wazi, na utashikilia kanuni za kujadiliana, kujenga na kunufaika kwa pamoja, pia kukaribisha ushiriki wa wenzi wote. Na China siku zote itakuwa mwenzi anayeaminika katika njia ya mafungamano ya kiuchumi ya dunia.