Jaribio lolote la kuingilia mambo ya Hong Kong na siasa za ndani za China halitafanikiwa
2019-07-02 20:48:23| CRI

Julai 1 ambayo ni maadhimisho ya miaka 22 tangu Hong Kong irudi China, baadhi ya watu wenye msimamo mkali walishambulia jengo la Bunge la Hong Kong, na kufanya uharibifu mbaya ndani ya jengo hilo. Tukio hilo la kimabavu limeathiri vibaya utawala wa sheria na kuharibu vibaya utulivu wa jamii ya Hong Kong, ambalo linalaaniwa na jumuiya ya kimataifa. Lakini Marekani, Uingereza na Umoja wa Ulaya zimetumia kisingizio cha uhuru na haki za binadamu kudai kuhakikisha haki za kupinga kwa njia ya amani. Kigezo tofauti cha kushughulikia uhalifu wa kimabavu ni kitendo kibaya cha kuingilia kati mambo ya Hong Kong na siasa za ndani ya China, ambacho kinalaaniwa na kupingwa kithabiti na serikali ya China.

Utawala wa sheria ni msingi muhimu zaidi wa Hong Kong. Mwezi wa Februari mwaka huu, serikali ya Mkoa wa utawala maalumu wa Hong Kong ilizindua marekebisho ya kanuni mbili za kazi kuhusiana na uhamishaji wa wahalifu wanaokimbia ambao lengo lake ni kushughulikia suala la uhamishaji la kesi husika na kuziba pengo la mfumo wa sheria ili kuepusha Hong Kong kuwa pepo ya wahalifu. Lakini sauti tofauti zimesikika katika jamii ya Hong Kong, baada ya kutokea kwa maandamano hata vurugu, serikali ya eneo hilo imeamua kusimamisha marekebisho ya sheria, ili kusikiliza maoni tofauti ya jamii na kuhimiza maendeleo ya utawala wa kisheria.

Lakini baadhi ya watu wenye msimamo mkali hawajasitisha vitendo vyao, kwa sababu lengo lao si kupinga marekebisho ya sheria, bali ni kuivuruga Hong Kong kwa kisingizio hicho na kutimiza malengo yao ya kisiasa yasiyoweza kuonekana. Walikusudia kuichagua Julai 1 ambayo ni siku ya kuadhimisha miaka 22 tangu Hong Kong irudi katika China kuzuia barabara, kuwashambulia polisi wa Hong Kong, na kuvamia jengo la baraza la sheria la ambalo ni alama ya sheria ya Hong Kong. Kitendo chao cha kimabavu kimezidi mstari wa mwisho wa kueleza madai yao kwa njia ya amani, na kuleta tishio kubwa kwa utaratibu wa Hong Kong.

Lakini nchi za magharibi zinazodai kiwango cha juu cha utawala wa kisheria zimekuwa na uvumilivu, huku zikidai kuhakikisha haki za kupinga kwa amani za wahalifu hao. Wamesahau jinsi serikali zao zinavyochukulia hatua kali dhidi ya waandamanaji wanaofanya mabavu. Wakati wahalifu walipolishambulia jengo la bunge la Hong Kong, nchi hizo zimechagua kuwa vipofu na kuunga mkono wahalifu hao.

Kitendo chao cha "vigezo viwili" kimekiuka sheria ya kimataifa na kanuni za msingi za uhusiano wa kimataifa na kuharibu usalama wa mamlaka ya China. China ina msimamo wazi na thabiti kwa uingiliaji kati wa nguvu ya nje: mambo ya Hong Kong ni siasa ya ndani ya China, nchi, mashirika ya nje na mtu yeyote hana haki ya kuingilia kati. Kama nguvu hizo hazitasitisha vitendo vyao, China itatakiwa kuchukua hatua zaidi.