Baada ya rais Xi Jinping wa China kutangaza hatua tano muhimu za kuharakisha hatua ya kupanua ufunguaji mlango kwenye Mkutano wa kilele wa kundi la G20, serikali ya China imeonesha nia thabiti ya kupanua ufunguaji mlango katika mkutano wa 13 wa Baraza la Davos la majira ya joto, na itakuza hatua ya ufunguaji mlango katika viwanda vya utengenezaji na utoaji wa huduma, kupunguza zaidi kiwango cha ushuru, kulinda kwa nguvu zaidi hakimiliki ya ubunifu, na kiwango cha ufunguaji mlango na uwazi kwa uwekezaji kutoka nje pia kitakuwa juu zaidi.
Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang akihutubia ufunguzi wa mkutano wa 13 wa Baraza la Davos la Majira ya Joto, ametangaza hatua mbalimbali kuhusu kupanua ufunguaji mlango, ambao ni utekelezaji halisi wa ahadi aliyotoa rais Xi Jinping katika mkutano wa kilele wa kundi la G20 kuhusu kupanua ufunguaji mlango.
Hivi sasa wakati hali ya kujilinda kibiashara na utaratibu wa upande mmoja inazidi kuenea, changamoto zinazuokabili uchumi wa dunia, na hali isiyotarajika inazidi kuongezeka, imani ya wawekezaji imezidi kupungua. Kutokana na hali hii, mkutano wa kilele wa kundi la G20 umeonesha ishara chanya, hususan hatua muhimu zilizotangazwa na rais Xi Jinping wa China kuhusu kupanua zaidi soko, uagizaji wa bidhaa, kuzidi kuboresha mazingira ya biashara, na kuhimiza mazungumzo ya uchumi na biashara, zimekaribishwa na kupongezwa na jumuiya ya kimataifa.
Naibu katibu mkuu wa Mkutano wa maendeleo ya biashara wa Umoja wa Mataifa Bibi Isabelle Durant amesema, hatua hizo zina umuhimu mkubwa, na zimeifanya dunia itambue msimamo wa China kuhusu kufungua mlango, pia zinasaidia utatuzi wa matatizo yaliyopo hivi sasa.
Chansela wa Ujerumani Bibi Angela Merkel pia amesema, ahadi kuhusu China kupanua ufunguaji mlango haitakuwa maneno tupu. Hali ambayo imeonesha kuwa, bila ya kujali mazingira ya nje yatakavyopata mabadiliko gani, kupanua ufunguaji mlango na kutimiza kusaidiana na kunufaishwa kwa pamoja zitakuwa miongozo thabiti ya China. China itazidi kuboresha mazingira ya biashara, na kutoa fursa nyingi zaidi kwa wawekezaji duniani, ili kujenga mazingira yanayoweza kutarajika kwa dunia yenye hali isiyoweza kutarajika.