Ushirikiano kati ya China na Marekani ni matarajio ya wananchi wa nchi hizo mbili
2019-07-04 19:28:49| CRI

Gazeti la Marekani Washington Post limetoa barua wazi kwa rais Donald Trump wa Marekani na bunge la Marekani. Barua hiyo iliyosainiwa na watu mia moja kutoka sekta ya taaluma, diplomasia, jeshi na biashara nchini Marekani, imeeleza ufuatiliaji kwa kupungua kwa uhusiano kati ya Marekani na China, huku ikiona hali hiyo hailingani na maslahi ya Marekani na Ulimwengu. Barua hiyo pia imesema, hakuna makubaliano ya pamoja ya kupambana kwa pande zote na China kwenye serikali ya Marekani, na kubainisha matarajio ya kuendeleza uhusiano huo kati ya nchi hizo mbili nchini Marekani.

Barua hiyo imeeleza baadhi ya maoni yenye maana: China si adui wa Marekani katika uchumi, vitendo vingi vya Marekani vimesababisha kupungua kwa kiasi kikubwa kwa uhusiano kati ya pande hizo mbili; Hatua nyingi za Marekani za kujaribu kutenganisha China na uchumi wa dunia zimeharibu hadhi na sifa yake, na kuleta hasara kwa maslahi ya uchumi wa nchi zote; ushiriki wa China una umuhimu mkubwa kwa mifumo wa kimataifa na ajenda za ulimwengu yakiwemo mabadiliko ya hali ya hewa, na njia nzuri zaidi kwa Marekani kulinda maslahi ya taifa ni kurejesha uwezo wa ushindani kwenye dunia inayobadilika kila siku na kushirikiana na nchi na mashirika mengine.

Barua hiyo imeonesha kuwa mkutano kati ya marais wa China na Marekani huko Osaka kufikia makubaliano kuhimiza uhusiano kati ya pande mbili juu ya msingi wa uratibu, ushirikiano na utulivu na kukubaliana kuanzisha tena mazungumzo ya uchumi na biashara juu ya msingi wa usawa, na kuheshimiana ni matarajio ya pamoja ya watu wa nchi hizo mbili, ambayo pia yanalingana na matarajio ya pamoja ya jumuiya ya kimataifa.

Kama barua hiyo inavyoeleza, China si adui wa Marekani katika sekta ya uchumi. Uhalisi wa uhusiano kati ya China na Marekani ni kunufaishana, thamani ya biashara za bidhaa za pande mbili imeongezeka kutoka dola zisizozidi bilioni 2.5 mwaka 1979 hadi dola zaidi ya bilioni 630 za kimarekani mwaka jana. Thamani ya jumla ya uchumi wa nchi hizo mbili imeongezeka hadi asilimia 40 ya uchumi wa dunia, mafanikio ya upande wowote kati ya China na Marekani yanategemea msingi wa mafanikio ya upande mwingine. Hatua ya kuongeza ushuru ya Marekani imeenda kinyume na msingi wa kunufaishana wa uhusiano wa pande mbili, na itaharibu maslahi za pande zote mbili.