Uongo wa baadhi ya wanasiasa wa Uingereza kuhusu mambo ya Hong Kong
2019-07-05 19:43:35| CRI

Hivi karibuni tukio la kimabavu ambalo watu wenye msimamo mkali walivamia jengo la baraza la sheria lilitokea huko Hong Kong. Baadhi ya wanasiasa wa Uingereza wametumia taarifa ya pamoja ya China na Uingereza ambayo haifanyi kazi tena kama kisingizio, na kudai kuwa wanaunga mkono wakazi wa Hong Kong kulinda "uhuru" uliopiganiwa na Uingereza na kuitaka serikali ya mkoa wa utawala maalumu la Hong Kong kutotumia tukio hilo la kimabavu kama sababu ya kutuliza hali. Madai hayo yasiyo na msingi wowote yanaunga mkono kidhahiri uhalifu na vitendo vya kimabavu na kuingilia kati mambo ya Hong Kong na siasa ya ndani ya China, ambayo yanaweza kuharibu uhusiano kati ya China na Uingereza.

Kwanza, taarifa ya pamoja ya China na Uingereza ni nyaraka ya kisiasa iliyosainiwa na pande hizo mbili mwaka 1984 kuhusu kurejesha mamlaka ya Hong Kong kwa China na mipango husika ya kipindi cha mpito. Baada ya Julai 1 mwaka 1997 Hong Kong kurudi katika China, haki na majukumu yote yanayohusiana na Uingereza katika nyaraka hiyo yaliisha, na nyaraka hiyo haifanyi kazi tena. Uingereza haina mamlaka, utawala na usimamizi kwa Hong Kong iliyorudi China, na pia haina majukumu ya kimaadili. Lakini baadhi ya watu wa Uingereza bado hawajaiacha nyaraka hiyo, kitendo hicho hakitokani na ujinga wa historia na siasa, bali ni kisingizio cha kuingilia kati mambo ya Hong Kong na siasa ya ndani ya China.

Pili, baadhi ya watu wa Uingereza wanadai kuwa uhuru wa wakazi wa Hong Kong unapiganiwa na Uingereza, huku wakisema uongo kwamba Hong Kong haina demokrasia halisi baada ya kurudi China. Lakini msomi wa Uingereza Bw. Martin Jacques amesema, madai hayo ni uongo wa mtindo wa Uingereza, wakati Uingereza ikiitawala Hong Kong wakazi wa huko hawakuona hata kivuli cha demokrasia. Baada ya Hong Kong kurudi katika China, serikali ya China inafuata katiba na sheria ya msingi ya Hong Kong na kutekeleza utaratibu wa "Nchi Moja na Mifumo Miwili" na "Watu wa Hong Kong kuitawala Hong Kong", wakazi wa huko wamekuwa watawala halisi na kuwa na haki za kidemokrasia na uhuru usiokuwepo awali.

Tatu, serikali ya mkoa wa utawala maalumu ya Hong Kong inashughulika tukio hilo la kimabavu kwa kufuata sheria na kanuni, uhalali wake hauna mashaka yoyote. Sheria ya msingi imewapatia wakazi wa Hong Kong uhuru na haki za kutoa maoni, kukusanyika na kuandamana. Lakini mtu yeyote anatakiwa kuheshimu haki za watu wengine na kutoathiri utaratibu na usalama wa umma, kutokiuka sheria na kufanya uhalifu wa kimabavu.

Miaka 22 imepita, Hong Kong imekuwa mkoa wa utawala maalumu wa China, sio koloni la Uingereza. Hivyo mambo ya Hong Kong ni siasa za ndani za China, nchi, shirika na mtu yeyote hana haki kuingilia kati.